"BOKO HARAM LIMEUNDWA NA WAMAGHARIBI"


Kiongozi wa jamii ya Waislamu wa Kishia nchini Nigeria Ibrahim Zakzaky amesema kuwa, kundi la Boko Haram limeundwa na kufadhiliwa na nchi za Magharibi kwa lengo la kufunika njama za Wamagharibi katika kupora utajiri wa Nigeria. Zakzaky ameeleza kuwa, suala la kupambana na Boko Haram halipo, bali kwa hakika operesheni hiyo inatekelezwa na nchi za Magharibi kwa lengo la kufunika uporaji utajiri wa Nigeria kwa kisingizio cha kuwasaka wafuasi wa kundi hilo. Pia sambamba na kuashiria mabadiliko ya hivi karibuni kaskazini mwa Nigeria na wimbi la mashambulizi ya Boko Haram kwenye eneo hilo, kiongozi huyo wa jamii ya Mashia nchini Nigeria amesema, suala hilo linashabihina na operseheni zilizofanywa na nchi za Magharibi huko Iraq na Afghanistan, kwani madola ya Magharibi yamefahamu kuna utajiri mkubwa wa dhahabu na platinum nchini Nigeria.
Wakati huo huo Ibrahim Zakizaky amekosoa ukandamizwaji wa wafuasia wake unaofanywa na maafisa wa usalama wa Nigeria kwa kisingizio cha kuimarisha usalama na kusema kuwa, hakuna sheria inayoruhusu watu kutiwa mbaroni bila kuhukumiwa.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, karibu Wanigeria milioni 6 ni wafuasi wa madhehebu ya Kiislamu ya Shia, ambao wengi wao wanaishi kwenye maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo ya Kano, Sokoto na Kaduna.