Vijana tunatakiwa kuungana na kuwa kitu kimoja
na sauti moja ili tuweze kutimiza malengo yetu ya Kueneza fikra sahihi
ya Uislamu aliyotuachia Mtukufu Mtume (s.a.w.w) tumeona mara nyingi
jinsi gani baadhi ya vijana wa Madhehebu nyingine na wasiokuwa
Waislamu wanavyojitolea katika vile wanavyoviamini kuwa ni sahihi na
wanafikia malengo yao, naamini kama na sisi tutapanga mikakati madhubuti
tunaweza kupiga hatua mbele zaidi, nadhani vijana wenzangu mtakuwa
mashahidi leo hii katika baadhi ya harakati zetu zinakuwa kwa kasi na
kuzolota yote kwa sababu hakuna ushirikishwaji wa vijana naamini kama
vijana tutasimama imara na kuwa sauti moja nadhani kazi ya kueneza fikra
za Ahlul-Bayt (a.s) itakuwa nyepesi mno na tutashinda vita dhidi ya
maadui wa harakati zetu na hakuna mtu atakayetuchezea, tusiwaachie
Masheikh tu hii ni kazi ya watu wote. Mwenyezi Mungu anasema: “Wale
walioamini na wakahama na wakapigania dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali
zao na kwa nafsi zao wana cheo kikubwa mbele ya Mwenyezi Mungu hao ndio
watakao tengenekewa.” (Qur’an: 9:20)
“VIJANA NI UTI WA MGONGO WA HARAKATI”
“VIJANA NI UTI WA MGONGO WA HARAKATI”