Taasisi
ya Bilal Muslim Mission imeanza upya harakati zake baada ya kukaa kimya
mda mrefu wameanza na ujenzi wa vituo vipya na ukarabati wa baadhi ya
majengo ya Bilal katika baadhi ya Mikoa kwa ajili ya kuanza kutoa elimu
ya dini ya Kiislamu kama ilivyokuwa
hawali, baadhi ya wanakamati wa taasisi hiyo wamesema itakuwa haibu sana
kuacha nguvu iliyotengenezwa na viongozi na Maulamaa waliyopita kabla
yao itoweke wamesema maadamu wapo hai watasimama kwa nguvu zote
kuhakikisha Bilal inarudi katika hali yake ya zamani pia wamemalizia kwa
kusema kuacha Bilal itoweke katika jamii ni kumfedhehesha Bilal Sahaba
wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w).