Miongoni mwa sifa ambazo ni lazima awe nazo Kiongozi ni uadilifu, na autumie katika pande mbili:
1- Katika uhusiano wake na Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa maana ya kwamba ni wajibu juu ya Kiongozi kumfanyia Mwenyezi Mungui uadilifu, Imam Ali bin Abi Talib (a.s) anasema: “Mfanyieni uadilifu Mwenyezi Mungu..” hivyo ni kwa kuilazimisha nafsi yake kumtii yeye, kutekeleza vipengele vya sheria na kutekeleza wajibu wake kiukamilifu kama mmoja katika jamii na kama Kiongozi, na kadhalika kuilinda nafsi yake isiweze kuasi na kujiingiza katika mambo ya kimada na starehe za maisha ya duniani, mambo ambayo yatamzuia kupagilia mambo ya raia na kutekeleza mahitaji yao ya dharura, Imam Ali (a.s) anamsifu Muumini Mchamungu kwa kusema: “Amejiambatanisha binafsi na uadilifu, na ukawa uadilifu wake wa kwanza ni kujiondolea utashi binafsi.”
2- Katika uhusiano wake na watu, ambapo majukumu ya Kiongozi ya kidini, kijamii na kiutu yanamlazimisha kuwafanyia uadilifu kivitendo raia na Ummah (uadilifu wa Kijamii), kuwafanyia raia wote bila ubaguzi kwa kuheshimu haki zao na kuwapa uhuru wao kamili, na kuwatimizia nyenzo za maisha mazuri, na kuwatazama kwa mtazamo mmoja bila kuelemea upande mmoja na bila ubaguzi. Imam Ali (a.s) anasema: “….Na wafanyie watu uadilifu kutokana na nafsi yako na kutokana na jamaa zako walio Makhsusi..” Hakuna ubora wala upendeleo isipokuwa kwa imani na Uchamungu. Mwenyezi Mungu anasema: “Hakika Mtukufu zaidi yenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni aliye na Takua zaidi yenu…” (Sura Hujurat: 13).
Hata Kiongozi hana ubora wa asili kuliko watu wengine, wanajamii wote wako sawa mbele ya kanuni, na wala Kiongozi hana kinga dhidi ya kanuni, bali kanuni inawajumisha watu wote, hivyo iwapo mtu atamshitaki atapaswa kusimama pamoja na mgomvi wake mbele ya Kadhi ili mwenye haki kati yao ajulikane, kwa sababu hukumu zinawahusu wote bila ubaguzi.
Imam Ali bin Abi Talib (a.s) anasema: “Na ikiwa mamlaka uliyonayo yanakusababishia majivuno au kiburi, angalia utukufu wa mamlaka ya Mwenyezi Mungu juu yako, na uwezo wake kwako, ambao usio uweza nafsini mwako, hilo litakushusha tama yako, na kuzuia ukali wako, na kurejesha yaliyojificha mbali na akili yako!”