Sheikh Abubakar Shariff anajulikana kwa jina la Makaburi ameuwa kwa kupigwa risasi nchini Kenya usiku wa kuamkia leo.
Jeshi la Polisi lilikuwa likimtuhumu Sheikh Makaburi kwa kueneza itikadi kali za kueneza misimamo mikali ya Kiislamu kwa vijana wa dini ya Kiislamu mjini Mombasa Pwani ya Kenya na kuchochea vitendo vya kigaidi.
Pia amekuwa akituhumiwa kwa kusajili vijana kwenda kujiunga na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab nchini Somalia, madai ambayo Sheikh Makaburi amekuwa akiyakanusha mara kwa mara.
Vijana wameanza kufanya vurugu katika Msikiti wa Majengo, Mombasa baada ya kupata taarifa za mauaji ya Sheikh Makaburi.
Taarifa za hawali za kifo cha Sheikh Makaburi zilitolewa Masjid Mussa (Masjid Shuhadaa) Msikiti ambao umekuwa kitovu cha vurugu kati ya Polisi na vijana wanaodaiwa kuhubiri na kufuata itikadi kali za dini ya Kiislamu.
Mpaka sasa inasemekana haijulikani nani aliyetenda kitendo hiki cha kinyama kwa Sheikh Makaburi.
Katika picha Jeshi la Polisi likiuchukua mwili wa Sheikh Makaburi.
Mwenyezi Mungu anasema katika Kitabu chake Kitukufu: “Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.” (Qur’an: 4:93)
“HAKIKA SISI SOTE NI WAJA WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA.”