Mwanachuoni maarufu aliyopo mjini Mombasa na Imam wa Msikiti wa Bakarani Sheikh Ali Bahero, ameshambuliwa na kwa kudungwa visu karibu na Msikiti wa Mussa na vijana waliojihami kwa mawe, visu na Silaha butu katika eneo la Majengo alipokuwa alipokuwa akiingia katika Madrasa kwa ajili ya kusomesha. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Afisa mkuu wa Polisi katika eneo hilo Jafrey Mayag ametoa wito wa kudumisha amani na utulivu kwa vijana wa Kisauni ambao wanadaiwa kupanga mashambulizi hayo yanayodaiwa kuwa ni ya kulipiza kisasi. Sheikh Ali Bahero alikimbizwa katika Hospitali moja iliyopo katika eneo la Kisauni akiugulia majereha makubwa na mabaya sana kutokana na kudungwa visu kichwani na karibu na jicho na picha za Televisheni zilimuonyesha Sheikh huyo akiwa amekaa chini huku ametapakaa damu zilizovuja toka kichwani. Juhudi zilizofanywa na wanahabari kataka kumuona Sheikh huyo na kufanya naye mahojiano ziligonga mwamba, baada ya wanafamilia na madaktari wake kuzuia kumuona kutokana na hali yake ilivyokuwa baada ya kufanyiwa upasuaji. Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema, vijana wanaoaminika kuwa wenye msimamo mkali wa kidini ndio waliomvamia Sheikh Ali Bahero na kumshambulia wakidai kuwa alihusika katika kuchochea uvamizi uliofanyika katika Masjid Mussa ambapo baadhi ya waumini waliuawa na Polisi. Sheikh Ali Bahero ni mmoja wa Masheikh wa ANSWARU SUNNA na anatofautiana kimtazamo na kiitikadi na kundi jingine la ANSWARU SUNNA lililokuwa likiongozwa na Marehemu Sheikh Aboud Rogo ambalo wafuasi wake wanapatikana katika Masjid Mussa, Misikiti ambao hivi sasa unaitwa Masjid Shuhadaa. Vita vinavyoendelea nchini Somalia baina ya kundi la Al-Shabaab na Serikali ya nchi hiyo ni moja ya mada zinazobishaniwa sana na Maulamaa nchini Kenya baadhi wakiunga mkono Al-Shabaab kuwa wamo ndani ya Jihadi, ilihali wanachuoni wengi akiwemo Sheikh Bahero anapinga kuwa hakuna vita vya Jihadi vinavyopiganwa baina ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe.
SHEIKH BAHERO ASHAMBULIWA KWA MAPANGA: