(1) Maana ya Jihadi.
(2) Wajibu wa Jihadi.
(3) Vigawanyo vya Jihadi.
1- MAANA YA JIHADI:
Jihadi maana yake ni kupambana kwa ajili ya kuulingania Uislamu, kueneza na kupanua utawala wake na nguvu yake au kuutetea kutokana na uadui wa maadui.
2- WAJIBU WA JIHADI:
Jihadi ni katika nguzo muhimu sana za dini na wajibu wake ni miongoni mwa dharura katika dini tukufu ya Kiislamu.
3- VIGAWANYO VYA JIHADI:
Jihadi imegawanyika sehemu mbili:
1. Jihadi ambayo inakuwa kwa ajili ya kuondoa vizuizi vinavyozuia kulingania Uislamu, kwa maana kwamba jeshi la Kiislamu linashambulia na kupigana na adui bila ya kuhujumiwa, na hiyo ni kwa ajili ya kuondoa vizuizi vya kutangaza na kueneza Uislamu na kunyanyua neno la haki na kusimamisha dini na kuwaongoza makafiri na washirikina na kuondosha shiriki na kuvunja masanamu (na kwa hakika lengo la jihidi ya kuanza sio kufungua nchi bali ni kutetea haki ya asili kwa watu ambao wamenyimwa haki kwa sababu ya ukandamizaji wa nguvu ya makafiri, washirikina na madikteta juu yao kutokana na uadilifu na kumwabudu Mwenyezi Mungu na kumpwekesha kwake.)
2. Jihadi ya kujitetea dhidi ya vizuizi na vikwazo kutokana na uadui wa maadui na hiyo ni pale maadui wanaposhambulia na kuhujumu nchi ya Waislamu na wanavuka mpaka wa ardhi yao kwa mabavu ya kisiasa au ubabe wa kijeshi au ukandamizaji wa kiutamaduni au wa kiuchumi.
1- JIHADI YA KUANZA:
1. Jihai ya kuanza haihusiani tu na zama za Nabii (s.a.w.w) au Imam Ma'asum (a.s), bali inajuzu kwa Faqihi mwenye kutimiza masharti ambae anaongoza mambo ya Waislamu anapoona masilahi yanahitajika hivyo kuamrisha jihadi ya kuanza.
2. Ahlul-Kitab (Wakristo na Wayahudi na Zardashitiyun) ambao wanaishi katika nchi za Kiislamu maadamu wanatii kanuni za dola ya Kiislamu ambayo wanaishi chini ya himaya yake, hukumu yao ni hukumu ya mwenye mkataba maadamu hajafanya yanayopinga amani (yaani nafsi zao na heshima zao na mali zao zinakuwa ni zenye kuheshimiwa na kuhifadhiwa na kulindwa haki zao za kisheria na kikanuni)
3. Kama makafiri wakishambulia nchi ya Kiislamu na Waislamu wakawateka baadhi yao basi hatima ya mateka wa vita iko mikononi mwa mtawala wa Kiislamu na sio haki kwa Waislam kama watu binafsi kupanga hatima yao, na hivyo haijuzu kwa yeyote kati ya Waislamu kummliki yeyote kati ya makafiri katika Ahlul-Kitab au wasiokuwa wao wanaume au wanawake, ni sawa iwe katika nchi ya kikafiri au katika nchi ya Waislamu.
2- JIHADI YA KUJITETEA:
(a). Kuutetea Uislamu na Waislamu ni wajibu na wala haihitajii idhini ya wazazi wawili lakini katika wakati huo huo inapasa kwa mwanadamu kufanya juhudi ya kupata ridhaa yao kadri inavyowezekana.
(b). Kama ikilazimu kuhifadhi nafsi yenye kuheshimika na kuzuia kutokea mauaji kwa kuingilia haraka na kwa moja kwa moja hiyo inajuzu, bali ni wajibu kisheria kwa mujibu wa wajibu wa kuhifadhi nafsi yenye kuheshimika, na hili halihitaji ruhusa ya mtawala au amri yake. isipokuwa kama kutetea nafsi yenye kuheshimika kuna sura nyingi zinazotofautiana hukumu yake kulingana na kuitalifiana kwake.
Kwa Mujibu wa Fatwa za Ayatullah Al-Udhuma Al-Imaam Sayyed Ali Hossein Ali-Khamenei.
Tuwaombee dua Waislamu wenzetu waliopo Afrika ya kati kutokana na mashambulizi wanayoyapata.