Kumbukumbu ya kifo cha Bibi Fatma Zahrau bint wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Fatima Zahrau amezaliwa kutokana na wazazi wawili watukufu, kwani hakuna mtu yeyote ambaye ana baba mwenye athari kama za baba yake, athari ambazo zilibadili sura nzima ya historia, huku ndani ya muda mfupi zikimpeleka Mwanadamu hatua za mbali kuelekea mbele. Wala historia haijatusimulia kuhusu mama kama mama yake ambaye alimpa Mume wake na dini yake tukufu kila alicho nacho kwa malipo ya kupata uongofu na nuru.
Chini ya kivuli cha wazazi hawa wawili watukufu ndipo alipokulia Fatima Zaharau, akakulia ndani ya nyumba ambayo imezungukwa na mapenzi ya baba yake ambaye alibeba joho la Utume na akavumilia yale ambayo majabali yaliwashinda kuvumilia.
Imepoakewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s) kuwa Mtume (s.a.w.w) amesema: “Hakika bint yangu amepewa jina la Fatima kwa sababu Mwenyezi Mungu amemtenga mbali na moto yeye na yule atakayempenda.
Rejea: Amalis-Suduq, Uk.484,
Al-Khiswal, Juz. 2 Uk. 414,
Dalailul-Imamah, Uk. 10,
Tajul-Mawalid, Uk. 20.