Hakika dini tukufu ya Kiislamu ambayo ndio
hitimisho la dini zote za mbinguni na yenye kubakia hadi siku ya Kiyama,
ni dini ya Sheria na kuendesha mambo ya jamii, na hivyo ni lazima kwa
jamii ya Kiislamu kwa tabaka zake zote kuwa na walii na
mtawala wa Kisheria na Kiongozi ili kuhifadhi Ummah wa Kiislamu
kutokana na Shari ya maadui wa Uislamu na Waislamu, na ili kuhifadhi
nidhamu yao na kusimamisha uadilifu na kuzuia mwenye nguvu kumuonea
mnyonge, na kuhifadhi njia za maendeleo na mabadiliko ya kiutamaduni,
kisiasa na kijamii.