Baadhi
ya Wanaharakati wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashariyyah, waliokutana siku
ya J.pili tarehe 16/02/2014 katika Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kuangalia
jinsi gani wataweza kufanya harakati za kueneza fikira sahihi za
Uislamu aliyotuachia Mtukufu Mtume
Muhammad (s.a.w.w) katika Mkoa huo pia walipata nafasi ya kutembelea
sehemu mbalimbali miongoni mwa sehemu walizotembelea Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Tanga,Hawzat Al Qaim Bilal Muslim Mission pia walimtembelea
Sheikh Muhammed Bakary wa Shamsul Maarifa, yote haya ni kutaka kujenga
umoja na upendo baina ya wanadamu.