Waislamu wamefanya kosa gani hata wakawa wanaandamwa kiasi chote hiki katika kila kona ya dunia. Huko Jamhuri ya Afrika ya Kati kila leo ni ukatili dhidi ya Waislamu. Huko Palestina kila leo ni jinai dhidi ya Waislamu. Huko Myanmar kila leo ni kuuliwa na kukandamizwa Waislamu. Huko Ulaya na Marekani kila leo ni kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu na Bwana Mtume Muhammad SAW.
Je ni udhaifu wa Waislamu? Je ni kutoshikamana na kuwa kitu kimoja? Je ni kujiweka mbali na mafundisho sahihi ya dini yao? Je ni kutokuwa na msimamo Waislamu wenyewe huku wanadai kupenda dini yao lakini wakati huo huo wanawakumbatia maadui wa dini yao ambao hawafichi chuki zao dhidi ya Qur'ani na Mtume wa Allah? Ni nini hasa? Ikiwezekana toa pia maoni yako kuhusu nini kifanyike.