"Jihadharini, kwa hakika fitna ninayoihofia sana mimi kwa ajili yenu ni fitna ya Banu Umayyah. Kwa kuwa hiyo ni fitna pofu yenye giza: Jambo lake limeenea. Na balaa lake limekuwa kwa sura makh'susi. Na wakapatwa na balaa humo wenye kuitambua haki. Balaa litamuepuka asiye jua. Namuapa Mungu kwamba mtawakuta Bani Umayyah ni watu waovu kwenu baada yangu kama ngamia jike mzee mwenye tabia mbaya, anang'ata kwa mdomo wake na anapiga kwa mkono wake na kupiga teke kwa miguu yake ya nyuma na anazuia kukamuliwa maziwa yake.
"Watabakia juu yenu mpaka hawatomuacha miongoni mwenu isipokuwa yule wa manufaa kwao, au asiye na madhara kwao. Balaa lao litaendelea juu yenu mpaka kiasi cha kuwa kuomba nusura kwa mmoja wenu dhidi yao ni kama kuomba nusura kwa mtumwa dhidi ya bwana wake na kwa mfuasi dhidi ya amfuataye, fitna yao mbaya na ya kuogopwa itakujieni na sehemu ya jahiliya, hakuna humo alama za muongozo, wala dalili ionekanayo. Sisi ni Ahlul-Bayt (watu wa nyumba ya Mtume) twaepukana na hayo, wala si wanusuru wa hayo. Kisha Mungu atakuondoleeni kama iondolewavyo ngozi kutoka kwa wenye kuambatana nayo kwa madhila, na kuwasukuma kwa mabavu, na kuwanywesha kikombe kichungu, hatowapa ila upanga, na wala hatowavika isipokuwa hofu. Hapo Makuraishi watataka hata kwa gharama ya dunia yote na yaliyomo humo ili wanione mimi japo kwa mara moja tu lau kwa kadiri ya muda ule wa kuchinjwa ngamia ili niwakubalie lile ambalo hivi sasa nawaomba sehemu tu lakini hawako tayari kunipa.