"Je
Bani Umayyah kunijua kwao hakujawazuia kuniaibisha? Je kutangulia
kwangu (kuubali Uislamu) hakujawaweka mbali wajinga na kunituhumu? Kwa
kweli aliyowaonya Mungu amewaonya kwa ufasaha zaidi kuliko ulimi wangu,
mimi ni mtoa hoja dhidi ya watokao nje
ya dini, na ni hasimu wa wavunjao ahadi na wenye shaka, na kwenye Kitabu
cha Mungu. Kwa Kitabu cha Mungu hupimwa yasiyo wazi. Kulingana na
yaliyo mioyoni waja watalipwa."