JUHUDI ZA MAREKANI ZA KUTAKA KUBADILI MLINGANO WA NGUVU NCHINI SYRIA:


Baadhi ya nchi za Magharibi hususan Marekani, zinafanya jitihada za kubadili mlingano wa nguvu katika mgogoro wa sasa nchini Syria hasa baada ya kufanyika duru mbili za mazungumzo baina ya wawakilishi wa Serikali ya Damascas na makundi ya waasi wanaoungwa mkono na nchi za Magharibi.

Nchi hizo zinataka kuhalalisha njama hizo kwa kutumia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hata hivyo Baraza la Usalama Alkhamisi ya juzi lilichukua uamuzi wa kuakhirisha kura kuhusu muswada mpya dhidi ya Syria hadi Jumamosi ya leo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Genady Gatilov amesema kuwa muswada huo uliotayarishwa na  baadhi ya nchi za Magharibi haukubaliki. Awali serikali ya Russia pia ilikuwa imetangaza kuwa rasimu ya muswada dhidi ya Syria haifai na kuwa mapendekezo yaliyotolewa na washirika wa nchi za Magharibi katika muswada huo ni ya upande mmoja na hayazingatii uhakika wa mambo.

Juhudi zinazokuwa zikifanywa na Marekani sambamba na mkutano wa Geneva 2 huko Uswisi zilionesha kuwa Washington ina nia ya kubadili mlingano wa nguvu katika mgogoro wa Syria. Vilevile wito uliotolewa na balozi wa zamani wa Marekani nchini Syria Robert Ford akiwataka magaidi wazidishe mashambulizi nchini humo na juhudi za serikali ya Washington za kutaka kutolewa azimio katika Baraza la Usalama dhidi ya serikali ya Damascus vyote vinatathminiwa katika mkondo huo.

Marekani inafanya jitihada za kuiarifisha serikali ya Damascus kuwa ndiye mhusika pekee wa hali mbaya ya sasa nchini Syria na inataka kutumia kisingizio hicho kwa ajili ya kupasishwa azimio kwa mujibu wa kipengee cha saba cha hati ya Umoja wa Mataifa kinachoruhusu utumiaji wa mashambulizi ya kijeshi. Japokuwa hadi sasa harakati na njama za nchi za Magharibi hususan Marekani dhidi ya Syria zimefeli, lakini Washington inataka kutumia Umoja wa Mataifa katika harakati zake kwa ajili ya kuhalalisha njama hizo. Awali nchi za Russia naa China zilipiga kura ya veto dhidi ya miswada iliyokuwa imependekezwa na nchi za Magharibi dhidi ya Syria katika Baraza la Usalama.

Juhudi nyingi za kieneo na kimataifa za kutaka kutatua mgogoro wa Syria zinafadhilisha kutumia njia za kisiasa na kujiepusha na utumia wa mabavu na nguvu za kijeshi. Marekani inapuuza juhudi hizo za kimataifa na inaendelea kuyapa misaada ya silaha za kisasa makundi ya kigaidi yanayopigana na serikali ya Syria. Msimamo huo wa Washington umeonesha tena kuwa Marekani hutumia masuala na ugaidi na haki za binadamu kwa ajili ya malengo yake.

Marekani inazungumzia hali mbaya ya kibinadamu huko Syria huku magaidi wa kitakfiri na Kiwahabi wanaoungwa mkono na Washington na serikali ya Saudi Arabia wakiendelea kufanya mauaji na jinai za kutisha nchini humo. Makundi hayo yenye misimamo mikali ya Kiwahabi yanawatumia raia wa Syria kama ngao katika vita na yanaua na kuchinja vijana, wanawake na hata watoto wadogo. Magaidi hao wa Kiwahabi wamefikia kiwango cha juu cha upotofu kiasi cha kupasua vifua vya wahanga wao na kutoa mioyo na kisha kuitafuna mbele ya kamera. Vitendo kama hivi viovu vinavyofanywa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani na washirika wake hususan Saudi Arabia, ndivyo vinavyozidisha machungu na mgogoro wa Syria. Hivyo kuna haja ya kuwepo mapambano ya kweli dhidi ya ugaidi ambayo ndiyo yanayoweza kukomesha mgogoro wa Syria na si misimamo ya kindumakuwili ya Marekaani na waitifaki wake.


 MSIKITI WA AL-AQSWA, MSTARI MWEKUNDU KWA WAISLAMU:

Sheikh Akrama Sabri, Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Palestina huko Quds inayokaliwa kwa mabavu amesema kuwa, Msikiti wa al-Aqswa ni mstari mwekundu kwa Waislamu. Sheikh Akrama Sabri  ambaye pia ni khatibu wa Masjidul Aqswa ametahadharisha kuhusu hatari na vitisho vya Wazayuni dhidi ya Msikiti wa al-Aqswa na kubainisha kwamba, eneo hilo takatifu ni mstari mwekundu kwa Waarabu na Waislamu. Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Palestina amesema kuwa, taifa la Palestina halitafumbia macho hata kipande kidogo kabisa cha ardhi ya Baytul Muqaddas; kwani Mayahudi hawana uhusiano wowote na ardhi hiyo. Aidha Sheikh Sabri ameukosoa vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kwa hatua zake za kuyavunjia heshima maeneo matakatifu ya Kiislamu hususan Masjidul Aqswa na kubainisha kwamba, mashambulio ya kila leo ya Wazayuni na walowezi wa Kiyahudi dhidi ya Msikiti wa al-Aqswa yanafanyika kwa lengo la kutwisha hali mpya na kuchochea hisia za Waislamu bilioni mbili ulimwenguni. (irib)