Saudia Arabia itatekeleza mpango wake wa kubomoa jengo la kihistoria la mahala alipozaliwa Bwana Mtume Muhammad SAW ikiwa ni sehemu ya mradi wa ustawi mpya. Mabuldoza yamewekwa tayari kubomoa jengo lililoko katika mji mtakatifu wa Makka katika mahala panapoaminika kuwa ndipo alipozaliwa Mtume SAW. Ubomoaji wa jengo lijulikanalo kama Nyumba ya Mawlid, ni sehemu ya mradi wa mabilioni ya dola wa kujenga jengo kubwa la kisasa karibu na Masjidul Haram, eneo takatifu zaidi la Kiislamu na mahala ilipo Al Kaaba, kibla cha Waislamu. Kwa mujibu wa wanahistoria, jengo la mahala alipozaliwa Bwana Mtume Muhammad SAW ndilo eneo pekee la kihistoria lililosalia nchini Saudi Arabia. Utawala wa kifalme wa Aal Saudi umeunga mkono mpango wa ustawi mpya kwa gharama za kufuta athari za majengo ya kale. Mnamo mwezi Aprili mwaka uliopita wa 2013 Mufti Mkuu wa Saudia Sheikh Abdul Aziz Bin Abdullah al-Sheikh alitetea mpango huo wa kubomoa turathi za zama za mwanzoni mwa Uislamu katika mji mtukufu wa Makka. Kiongozi huyo mkuu wa kidini nchini Saudi Arabia alifika mbali zaidi hata kuelezea ubomoaji huo kuwa ni jambo la lazima. Kitendo cha kubomoa jengo la kihistoria la mahala alipozaliwa Bwana Mtume SAW kinatazamiwa kuamsha hasira za Waislamu wanaokwenda nchini Saudia kutekeleza ibada ya Hijja…/Chanzo cha habari: http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/38367-saudia-kubomoa-jengo-la-mahala-alipozaliwa-mtume-saw
JENGO LA MAHALA ALIPOZALIWA MTUME S.A.W KUBOMOLEWA: