Sheikh Abdul Malik (kushoto) amepokea Vitabu
takriban mia mbili (200) vya dini ya Kiislam kutoka kwa Mwenyekiti wa
Al-Itrah Foundation jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kwenda
kuendeshea harakati wilayani Bukoba, taasisi ya Al-Itrah imekuwa
ikifanya harakati za ugawaji wa vitabu mbalimbali vya dini ya Kiislamu
katika jamii kwa ajili ya kuifanya jamii itambue huwepo wa Mwenyezi
Mungu (s.w.t) na kuitambua haki kupitia kizazi cha Mtukufu Mtume
Muhammad (s.a.w.w).