MWISHO MBAYA WA "CHINJACHINJA WA SABRA NA SHATILA"


Mimi sijui chochote kuhusiana na kile kinachojulikana kama misingi ya kimataifa, lakini ninaahidi kwamba, kila mtoto wa Kipalestina atakayezaliwa katika Mashariki ya Kati nitamchoma moto. Wanawake na watoto wao ni hatari zaidi kuliko wanaume wa Kipalestina; kwani uwepo wa mtoto yeyote wa Kipalestina maana yake ni kuendelea kuongezeka kizazi cha Wapalestina. Haya ni matamshi ya Ariel Sharon aliyoyatoa mwaka 1956 katika mazungumzo yake naOuze Merham, jenerali wa Kizayuni. Hatimaye baada ya miaka minane ya kuishi kidhalili katika koma, Ariel Sharon "chinjachinja wa Sabra na Shatila" ameaga dunia. Habari ya kuaga dunia katili Sharon akiwa na umri wa miaka 85 ilitangazwa adhuhuri ya jana na Radio ya Kizayuni. Ukweli wa mambo ni kuwa, umri wa Sharon ulikuwa umefikia tamati tangu Januari mwaka 2006 baada ya kupata mshituko wa ubongo na aliyendelea kuishi katika koma kwa msaada wa vifaa vya kitiba. Wazayuni walikuwa wamempatia Sharon lakabu ya buldoza wakikumbuka masiku ambayo Sharon alikuwa Waziri wa Kilimo na kwa amri yake nyumba za Wapalestina zikibomolewa na mashamba yao kuharibiwa ili nafasi yake kujengwe vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi. Hata hivyo Wapalestina kwa upande wao wanamtambua katili Sharon kwa jina la "chinjachinja" wakikumbuka kipindi ambacho Sharon alikuwa Waziri wa Vita wa Israel na kwa amri yake Lebanon ikakaliwa kwa mabavu na kilichofuatia ni kuuawa kwa umati Wapalestina katika kambi za wakimbizi za Kipalestina za Sabra na Shatila katika viunga vya Beirut mwaka 1982 na kwa muktadha huo ulimwengu ukakumbwa na msiba na majonzi makubwa. Historia itahifadhi milele tukio chungu la maafa ya Sabra na Shatila kwani katika tukio hilo, zaidi ya wanawake, watoto, vijana na wazee wa Kipalestina elfu mbili waliuawa kwa umati na mamluki wa kifalanja wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Kama vile haitoshi, ukatili wa mafalanja na Wazayuni ulidhihiri zaidi pale walipoamua kucheza na kunengua mbele ya maiti za Wapalestina walizoziua kinyama. Kwa hakika mauaji ya Deir Yassin, Kafr Qasim na Sabra na Shatila ni miongoni mwa maafa ya kutisha kabisa katika karne ya 20 ambayo hayatasahauliwa. Mwaka 1982, Sharon akiwa Waziri wa Vita wa utawala haramu wa Israel aliongoza vita dhidi ya Lebanon na mwaka 1983 alikabiliwa na mashanikizo makubwa ya fikra za waliowengi ulimwenguni kutokana na mauaji yake ya umati dhidi ya Wapalestina katika kambi za wakimbizi wa Kipalestina za Sabra na Shatila na hivyo akauzuliwa kutoka katika wadhifa wake huo. Hata hivyo Sharon alichomoza tena katika uga wa siasa za Israel mwaka 1990 akiwa Waziri wa Nyumba na kufanikiwa kujenga nyumba laki moja na arobaini na nne elfu katika maeneo ya Wapalestina kwa ajili ya walowezi wa Kiyahudi na kutokana na sababu huyo akapewa lakabu ya "Baba wa Harakati ya Ujenzi wa Vitongoji vya Walowezi wa Kizayuni." Katika uga wa siasa, Sharon ni mwasisi pia wa vyama viwili vya mrengo wa kulia vya Likud na Kadima. Mwaka 1998 Sharon akawa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Israe na mwaka 2000 aliingia katika Msikiti wa al-Aqswa na kulivunjia heshima eneo hilo takatifu, kitendo ambacho kilizua hasira na ghadhabu za Wapalestina na kupelekea kutokea Intifadha ya Pili. Mnamo mwaka 2001 Sharon akawa Waziri Mkuu wa Israel. Katika kipindi cha kuwa kwake Waziri Mkuu, chinjachinja huyo wa Sabra na Shatila aliongoza mpango wa ujenzi wa ukuta wa kibaguzi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan lengo likiwa ni kupora zaidi ardhi za Wapalestina. Kifo cha Ariel Sharon kimepelekea kufungwa faili jingine la mwasisi wa kukaliwa kwa mabavu Palestina. (irib)


 IRAN YALAANI JINAI ZA UTAWALA WA KIZAYUNI WA ISRAEL:

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina. Bi Marzie Afkham amesema leo kuwa, Iran inakihehasabu kitendo hicho cha Israel kuwa ni kinyume cha sheria na ni uvamizi. Ikumbukwe kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umeamua kujenga vitongoji zaidi vya Wazayuni katika ardhi unazozikalia kwa mabavu za Wapalestina. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa, Tehran inautaka Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu kuchukua hatua kali za kukabiliana na jinai na uvamizi huo wa Wazayuni na kuilazimisha Israel ikomeshe ujenzi wa vitongoji hivyo. Vile vile amesema, uamuzi huo wa utawala wa Kizayuni wa kuendelea kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina unazidi kubatilisha mazungumzo ya mapatano kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Mamlaka ya Ndani ya Palestina. Wizara ya Nyumba ya Israel siku ya Ijumaa ilitangaza kuwa, kuna mpango wa kujengwa nyumba 801 mpya za Wazayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na nyumba 600 nyingine huko mashariki mwa mji wa Baytul Muqaddas.


WAPALESTINA KUTOITAMBUA ISRAEL KAMA NCHI YA KIYAHUDI:

Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa hataitambua Israel kama nchi ya Kiyahudi.

Abbas alisema hayo jana akiwahutubia maelfu ya Wapalestina huko Ramallah katika Ukingo wa Magharibi na kuongeza kuwa, Wapalestina hawataacha takwa lao la kufanywa eneo la Quds Mashariki kuwa mji mkuu wa nchi huru ya Palestina. Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina aidha amesisitiza kuwa, hatakubali suluhisho lolote litakaloshindwa kufanikisha takwa hilo.

Wakati huo huo Catherine Ashton Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa, vitongoji vya Israel vinavyojengwa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ni kinyume cha sheria na kikwazo kikuu cha kupatikana amani katika Mashariki ya Kati. Ashton pia ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe ujenzi wa vitongoji hivyo. (irib)