JIANDAE KUPATA KITABU KIPYA HIVI KARIBUNI.


Taasisi ya Al-Itrah, iliyopo jijini Dar es Salaam inatarajia kutoa Kitabu mwezi ujao kilichobeba jina la "SHUJAA ALIYELIPIZA KISASI DHIDI YA WAUAJI WA IMAM HUSSEIN HAPO KARBALA (61'67 AH)." (MUKHTAR)

Mukhtar: Mtu aliyelipa kisasi kwa kupigana na kuwaua wale vinara wote walioshiriki katika mauaji ya mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) Imam Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala.
Jina lake kamili ni: Mukhtar Abu Ubaida Masuud Thaqafi kutoka katika kabila la Banu Hawazin. Alizaliwa mwaka wa kwanza wa Hijiria.
Mama yake alikuwa akiitwa Husna, (riwaya nyingine zinasema aliitwa Hilya). Baba yake aliitwa Abu Ubaida Thaqafi.
Alikuwa na dada yake mmoja jina lake Safia aliyekuwa mke wa Abdullah bin Umar, mtoto wa Khalifa wa pili, Umar bin Khattab. Dada yake mwingine alikuwa mke wa Umar bin Saad, Kamanda wa jeshi la Yazid katika Karbala. Mmoja wa bint zake aliolewa na Imam Zaynul Abdin (a.s) na wakapata mtoto aliyeitwa Umar.
Kutokana na kazi yake maalumu aliyofanikiwa ya kulipa kisasi cha maadui wa Imam Hussein (a.s), zilizuka habari nyingi za kupotosha kuhusu maisha yake kwa wakati ule, kwa mfano, watu walidai alitoka katika familia duni isiyostahiki kuheshimika, n.k., bali yeye alitoka katika kabila tukufu la Banu Hawazin, ambapo pia walitoka watu watukufu kama utakavyoona ndani ya kitabu hiki pindi kitakavyokufikia ndugu msomaji.