"KUWAKUMBUKA MAULAMAA NI KUYAWEKA MAFUNDISHO YAO HAI"


Tanzania tunaitaji Kiongozi mahiri na jasiri kama Ibrahim Zakzaky, Kiongozi mwenye hofu na nchi za kibeberu hafai katika jamii leo hii tunaona baadhi ya watu na wanajiita Wanaharakati wanajaribu kuficha asali za Uislam nakuogopa kusema kweli pindi wanapoona dhuluma inatendeka kwa kuhofia kifungo na kifo, tumeshuhudia hivi karibuni katika baadhi ya maeneo wakipinga kusimamishwa picha za Maulamaa kwa hofu juu ya mataifa makubwa ya kibeberu kuwa wataweza kuonekana wanaunga mkono upinzani uliyopo baina ya kikundi cha Moqawama (Hizbullah) wanaoupigia kelele utawala halamu wa Israeli tujiulize je, leo hii nani anayesitahiki kunyanyua sauti dhidi ya dhuluma zinazofanywa ulimwenguni?.
 "Haki hiko wapi hali ya kuwa picha za maulamaa zinafichwa chini ya uvungu wa kitanda."