TANGAZO.

Tunapenda kuwakaribisha Waislam wote na kwa kila mpenda haki katika matembezi ya siku ya Ashura, Kwa ajili ya kuadhimisha Maombolezo ya Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), aliyetoa huai wake kwa ajili ya Ukombozi wa Mwanadamu kutokana na dhulma au kwa ibara nyinge alijitoa Muhanga kwa ajili ya kuubakisha Uislamu Sahihi wa babu yake, matembezi hayo ya amani yatafanyika siku ya Alhamisi Tarehe 14/11/2013 Saa 3:00 Asubuhi kuanzia Soko la Kigogo Sambusa hadi Masjid Al-Ghadiir, Kigogo Post,Dar es Salaam. Fikisha Ujumbe kwa wengine Insh’allah.

Imam Khomein katika usia wake anasema: “Kamwe msikubali yeyote yule kwa jina la ‘usasa na usomi’ kusema kuwa kutoa machozi na kuomboleza kwa ajili ya Masaibu ya Karbala ni Upuuzi.”

“Bila shaka kuwalilia Mashahidi ni kuyaweka mafunzo yao hai, ni njia ya kula kiapo cha kuuweka hai ujumbe wao.”