HAWZATUL AL-IMAM SAADIQ (A.S), YAFANYA USAFI KATIKA BARABARA YA KIGOGO,JIJINI DAR ES SALAAM.

Diwani wa kata ya Kigogo, jijini Dar es Salaam, amepongeza juhudi zilizofanywa na Wanaharakati wa Hawzatul Al-Imam Saadiq (a.s), katika usimamizi wa Mazingira katika Sehemu ya Kigogo, pia amesema ataonyesha ushirikiano wake katika Maombolezo ya Kifo cha Mjukuu wa Mtume (s.a.w.w), hususani katika matembezi ya amani yatakayofanyika siku ya Alhamisi pia atashiriki program ya kuchangia damu salama itakayofanyika siku hiyo baada ya matembezi .

 Katibu mkuu wa Harakati za kueneza fikra za Ahlul-Bayt (a.s), Sheikh Mohammad Abdi, akizungumza na waandishi wa habari Madhumuni ya kufanya usafi katika kata ya Kigogo amesema Imam Hussein (a.s), katika mambo aliyokuwa akipigania ulikuwa usafi na amani baina ya Wanadamu ulimwenguni.

 Wanaharakati wa Hawzatu Al-Imam Saadiq (a.s), wameitikia wito wa Imam Hussein (a.s) kwa kusafisha Mazingira katika kata ya Kigogo, wamesema program hiyo itakuaendelevu.

 Sheikh Kabwe, Mwalimu wa Hawzatu Al-Imam Saadiq (a.s), akionyesha ushirikiano katika usimamizi wa Mazingira kwa maana Uislam siku zote unaamrisha usafi wa Mazingira kwa Wanadamu.

 Wanafunzi wa Hawzatu Al-Imam Saadiq (a.s), iliyopo Kigogo Post, jijini Dar es Salaam wakifanya Usafi katika barabara ya Kigogo kwa ajili ya maandalizi ya Matembezi ya Maombolezo ya Imam Hussein (a.s) yatakayofanyika siku ya Alhamisi ya 14/11/2013.