MSIMAMO WA AHLUL-BAYT (A.S).

Imam Hussein (a.s) alishuhudia kwamba ni wakati ambapo watu binafsi na halikadhalika Ummah mzima na jamii ulikuwa umefungwa na utumwa na hivyo akaamua kuifungua minyororo hii ya ufungwa na kwa kuuawa shahidi yeye mwenyewe ameihuisha heshima ya Ummah iliyokufa, na mpaka siku ya Hukumu ameonyesha njia ya Ukombozi kwa Ubinadamu na kuwapa Ukombozi kutokana na utumwa.

 Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s) walipinga njama hizi khabithi za kibani Umayyah na mbinu zao za kishetani na walisimama kidete kwa nguvu zote walizokuwa nazo, kupambana na wimbi hili hatari na bida’a mbaya kabisa. Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s) walitangaza kwa sauti kubwa mtu kujiepusha na kushughulikia haja zake siku ya Ashura, na kugoma kufanya kazi siku hiyo na kuifanya kuwa ni siku ya huzuni na kulia na kumshutumu yule anayeitazama kuwa ni siku ya Baraka na kumuombea afufuliwe siku ya Kiyama pamoja na wazushi wa bida’a hii ya kishetani ambao ni Banu Umayyah na wafuasi wao.
 

Amri kutoka kwa Maimamu kuhusu kuweka msiba siku ya Ashura kwa kulia na kuamrisha wanafamilia kulia na kukuna kwa kulia….ni amri zilizotiliwa mkazo ambapo Imam anampa dhamana anayetekeleza hilo Pepo. Kinyume na madai ya kuwepo Baraka kwa kuweka na kununua chakula cha mwaka mzima siku ya Ashura, Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s) wanalaani na kufichua njama za mti uliolaaniwa (Banu Umayyah) na Wanazuoni wao. Lengo hasa la maadui hawa wa kizazi cha Mtume (s.a.w.w) ni kuwapotosha watu na kufunika tukio la huzuni na unyama walioufanya kwa kumuua kikatili Bwana wa Vijana wa Peponi, Imam Hussein (a.s), kipenzi cha Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) na hivyo kuepuka lawama na laana za Waislamu kwa kuwashughulisha na sherehe na kutabaruku. Waislamu kuliko kuhuzunika na kulia kama alivyofanya Mtume (s.a.w.w), watu wa nyumba yake, Masahaba wema na Waislamu kwa kifo cha Imam Hussein (a.s), bali pia mbingu na ardhi na vilivyomo vililia kwa msiba huu adhimu, wanasheherekea na kufurahi kwa kufuata uzushi wa Banu Umayyah! Mwenyezi Mungu apige mhuri nyuso zao kama alivyopiga nyoyo zao.