SAYYID HASAN NASRULLAH:KUONA PICHA YA IMAM MUSA SADR ILINIVUTIA KUWA MWANAFUNZI WA DINI.


Ripoti ya ABNA-....Sayyid Hasan Nasrullah katika maongezi yake na vyombo vya habari alidhihirisha mapenzi yake kwa Imam Musa Sadr na kuwa kwake Mwanafunzi wa Dini.
Mkuu wa kundi la Hizbullah Lebanon Hujjatul islam wal muslimin Sayyid Hasan Nasrullah katika maongezi yake na vyombo vya habari alieleza vipi alikuwa Mwanfunzi wa Dini.
Sayyid Hasan Nasrullah katika sehemu tofauti hakuficha mapenzi yake kwa Imam Musa Sadr akisema:mimi kuanzia utotoni mwangu nilikuwa na mpenda, na katika miaka hiyo nilisafiri na Baba kuelekea kusini mwa Bairut, na safari hiyo ilikuwa ni ya kikazi katika sehemu za mashia ambapo tuliishi na Baba katika Mkoa huo wa kifakiri. Siku miongini mwa siku nilienda Dukani kwa Mzee mmoja wa kishia Mzee huyo alikuwa amebandika picha ya Imam Musa Sadr ukutani, kuona picha hiyo nilimuuliza Mzee huyo ninani huyu yupo kwenye picha Uso wake una’gaa na kuvutia?! Mzee alinijibu huyu ni Imam Musa Sadr kiongozi wa mashia wa Lebanon na akanieleza zaidi kunako Imam Musa Sadr, kuanzia muda ule niliweka dhamira kuwa kama yeye na kuvaa nguo kama alizovaa.
Sayyid Hasan Nasrullah alipata Diplom alipokuwa na Umri wa miaka 16 na katika mwaka huo, na alijiunga na Chuo cha Dini cha Najaful Ashraf kusoma masomo ya Dini.pia alisoma katika Chuo cha Dini cha Al-Imamul Muntazar katika Mkoa wa Bal-ak pia katika Chuo cha Qum Jamuhuri ya kislamu ya Irani.
Alipokuwa na Umri wa miaka 21 Imam Khomein alimteuwa kuwa wakili wake katika mas-ala za kisheria katika Nchi ya Lebanon. Habari kutoka http://abna.ir/data.asp?lang=17&Id=261731