Hujuma hiyo nzito ilitokea wakati
Mashia hao wakiwa katika kuomboleza tukio la kuuawa kwa Husein bin Ali bin
Abitwalib ambaye ni mjukuu wa mtume Muhammad na ni kiongozi wa pili wa uislamu
baada ya mtume kwa mujibu wa itikadi za Mashia, ambapo aliuliwa na Shirm kwa
amri ya Yazid ambaye alikuwa kiongozi wa uislamu kwa wakati ule.
Hujuma hii ya jeshi la Bahrain
ambapo askari walitumia mabomu ya machozi imesababisha watu wengi kujeruhiwa
ambapo waathirika wengi ni wanawake na watoto.