Ayatullah Ali Khamenei:Imam Khomain ni shakhsia kumbwa
katika wanazuoni na si rahisi kupata mtu mwenye sifa kama imam Khomain kuwatoa
Manabii na Maimamu maasumina...alikuwa akikaa mbali na watu kwa ajili ya
kumuabudu mola wake na kumlilia, mtu ambae maadui wa Irani walikuwa wakimuogopa
ila katika swala ubinadamu hakuna mwenye huruma kama yeye.
Shahid
Mutahariy:wito wa Imam Khomain ulitikisa ulimwengu ambapo karne 14
zilizopita hakukutokea kitu kama hicho, Imam utadhani kuwa alikishuhudia
vita ya Badr, Uhud, Taabuk, Hunain, Khaibar na....
Muujiza wa imam katika kutabiri mambo
Utabiri
wa Imam ni barua kwa Gorbachof Mkuu wa umoja wa sovieti kumueleza kuwa
makini na wa mgharibi, na kama angetekeleza ushauri na nasaha Imam
yasingelimkuta yaliomkuta na kusambaratika umoja huo.
Ayatullah
Misbah Yazdiy:moja mwa faida za harakati ya Imam Khomain ni kuzagaa
uislamu Ulimwenguni na Dini zengine kuamka kama Ukristo kwa kurudi kwao
nyuma.
Sauti ambayo iliyotikisa Ulimwengu
Profesa
Hamid Maulana:kwa imani yangu hakuna sauti ilotikisa Ulimwengu katika
Karne ya 20 kama ilivyotikisa sauti ya Imam Khomain, Imam Khomain niwa
kwanza kuvunja rekodi ya kukalisha kimya wa Babe wa Dunia katika Vita ya
Dunia ambapo hapo ilikuwa haijawahi kutokea hapo kabla.
Site na Siasa
Dr.Shamiliy:kwa
hali ya sasa kuangalia kwa ufupi site Google utapata zaidi ya site
20100 zinazomzungumzia Imam Khomain na zaidi ya site 10776 zenye anuani
ya Imam Khomain zinazungumzia mambo tufauti, na utapochunguza site hizo
utakuta zaidi ya site 52000 zinazomzungumzia Imam Khomain zipo chini ya
mayahudi kila siku zikisambaza fikra mbaya dhidi ya Imam Khomain.
Kubadilika mbinu za uislamu baada ya mapinduzi ya Irani
Baada
ya ushindi wa mapinduzi ya kiislamu ya irani baada ya miaka 100 mbinu
za uislamu zilibadilika kuathirika na mapinduzi hayo kuzagaa uislamu
Mashariki na Magharibi Kusini na Kaskani mwadunia kunawafanya wa Krisko
kuamka kwani kila siku waislamu wanazidi kuongezeka idadi na kuzidi
kupungua idadi ya wa Kristo katika Nchi za ulaya na hasa Marekani, na
kupungua idadi kila mwaka ya wa Kristo sababu yake mapinduzi ya kiislamu
ya Irani.