Kwa maneno ya Imam Khomeini aliposema, kulia katika maombolezo ya Imam Husain (a.s) kunaweka hai mapinduzi na mwamko wake kwa maana ya kwamba, jamii ya watu wachache wanaweza kusimama imara kukabiliana na dola kubwa yenye nguvu. Maadui wanaogopeshwa na maombolezo hayo kwani maombolezo hayo ni maombolezo ya madhulumina, ni mayowe ya waliodhulumiwa mbele ya dhalimu.