JESHI LA SYRIA LINALOSAIDIWA NA HIZBULLAH WAMEURUDISHA MJI MUHIMU WA KARIBU NA DAMASCUS.


Vikosi vya syria vinavyosaidiwa na wapiganaji wa Hizbullah, na vikosi vingine vinavyounga mkono serikali wameuchukua tena mji uliokuwa kichaka cha waasi kusini mwa mji mkuu damascus Alhamisi wiki hii.

Urudishaji wa mji huo umeripotiwa na vikundi vya uchunguzi pamoja televisheni ya taifa ya syria.
Upatikanaji wa mji huo wa Sbeineh, uliokuwa makao muhimu ya waasi kusini mwa damascus, kumekuja siku tisa tu tangu kuanza kwa operesheni kubwa ya jeshi la syria la kukata njia ya msaada itumiwayo na waasi kupata msaada kutoka kwa washirika wao kupitia kusini mwa damascus, kwa mujibu wachunguzi wa haki za binaadamu wa syria ‘’sbeineh ulikuwa ni moja ya miji muhimu kwa waasi nje ya viunga vya mji wa damascus’’, alisema Rami Abdel rahman ambaye ni mkurugenzi wa kikundi chenye makao yake makuu huko Uingereza.
’’waasi huko kusini kwa sasa wamekatikiwa na misaada yao yote’’, aliongeza
Televisheni ya taifa pia imeongeza
‘’jeshi likisaidiwa na wapiganaji mahiri wa Hezbollah, vikundi vya wazalendo wa syria wana kikosi wa kishia wa syria wajulikanao kama Abul fadhli Al-abbas brigade. Ndio walioongoza oparesheni hiyo.

Kaburi la Sayyida Zainab(a.s) mjukuu wa mtume muhammad (sa.ww) ni sehemu muhimu sana kwa waislam wa shia ambayo ipo kusinimashariki mwa damascus.
Wapiganaji wa Hezbollah na vikosi vya shia kutoka Iraq ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiwasaidia wananchi wa syria kujilinda pamoja na kulinda maeneo matukufu kwa sasa wanapigana bega kwa bega kulinda sehemu za hizo za heshima na makaburi matukufu huko kusini mashariki mwa damascus.