SHEREHE YA EID AL - GHADIIR, IMEFANYIKA CHUO KIKUU CHA JAMIATUL MUSTAPHA, UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM,TANZANIA.


Sheikh Ali Juma Mayunga, akielezea Tukio la Al-Ghadiir jinsi ililivyokuwa siku ambayo Mtukufu Mtume Mohammad (s.a.w.w) alitamka maneno yafuatayo " Mimi ninakuachieni tiku ambacho mkishikamana nacho hamtapotea baada yangu, kimojawapo ni kikubwa zaidi kuliko kingine nacho ni Katabu cha Mwenyezi Mungu, ni kamba iliyonyooshwa kutoka juu mpaka chini. Na Kizazi changu Watu wa Nyumbani kwangu, havitaachana mpaka vinifike katika Haudh."

Rejea Sahihi Muslim J.4 Uk. 1873, Tarekh Bughdad J.8 Uk. 442, Addurrul Manthur J.2 Uk.107, Tafsirul Kabir J.8 Uk.163, Jamiul Usul J1 Uk. 187


Kwa kweli Tukio la Ghadiir Khom ni tukio lililobeba ujumbe mkubwa ambao waandishi wa Historia wanaona kuwa ni hitimisho la kazi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alioagizwa Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu kuufikisha kwa watu wote.
Tukio la Ghadiir Khom ni ukweli wa historia uliothibiti ambao hautiliwi shaka na watafiti wa historia. Ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w) baada ya kumaliza Ibada yake ya Hijja, wakati akirudi, alipofika Mahala paitwapo Ghadiir Khom. Ilikuwa tarehe kumi na nane mfungo tatu mwaka wa kumi Hijiria, alipofika Ghadiir Khom njia panda ziendazo Madina, Misri na Iraq.

Ikawa dharura juu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kutangaza jambo muhimu la atakaeshika Uongozi baada yake. Kwa fursa hii ambayo Waislam walijumuika zaidi ya laki moja, mkusanyiko ambao hautatokea tena utakaowajumuisha Waislam pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w). Na kwa fursa hii hii, Waislam kwa pamoja waweze kutoa Kiapo cha utii kwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s) Mwenyezi Mungu akateremsha Aya "Ewe Mtume! Fikisha uliyotemshiwa kutoka kwa Mola wako, na kama hukufikisha, basi hukufikisha ujumbe wake."
(Qur'an: 5:67). Hapo ndipo Mtukufu Mtume (s.a.w.w) akasimamisha msafara wake, waliokuwa mbele wakarudishwa, waliokuwa nyuma wakangojewa. Wote wakakusanyika pamoja. Mtukufu Mtume (s.a.w.w) akawasomea Aya hiyo, kisha akawauliza: "Katika watu, ni nani aliye bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao? Wote pamoja wakajibu: "Ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake tu ndio wajuao. Mtume akasema: " Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Kiongozi wangu, na mimi ni Kiongozi wa Waumini, na mimi ni mbora zaidi kuliko nafsi zao. Kisha akazema: Ambae mimi ni Kiongozi wake, basi huyu Ali ni Kiongozi wake.
Ewe Mola! Muunge atakae muunga (Ali) na mtenge atakaemtenga (Ali)....."
Waislam wote wakatoa kiapo cha Utii kwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s).

Rejea: Ihqaaqul Haqqi J.6 Uk.225 - 304, Al-Isaba J.1 Uk.305, Tarekh Bughdad J.8 Uk. 290, Tafsirul Kabiir J.12 Uk.49




 Madhehebu mbalimbali ya Kiislam wakiwa Chuo Kikuu cha Jamiatul Mustapha kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kukumbuka tukio la Al - Ghadiir (yaliyojili katika Hijjah ya mwisho ya Mtukutufu Mtume Mohammad s.a.w.w).

 Kushoto Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislam Tanzania, Sheikh Mohammad Abdi, akibadilisha Fikra na Sheikh Kabwe katika Sherehe ya Eid Al-Ghadiir iliyofanyika Chuo Kikuu cha Jamiatu Mustapha, Upanga jijini Dar es Salaam.