MWALIKO.


Bismillah Ta'alah.

Tunapenda kuwakaribisha Waislam wote katika sherehe ya Eid Al-Ghadiir itakayofanyika siku ya Alhamisi tarehe 24/10/2013, Masjid Al-Ghadiir, Kigogo Post, Dar es Salaam, Tanzania, kuanzia Saa 7:30 mchana hadi Saa 9:30 mchana. Fikisha ujumbe kwa wengine Insh'allah.

Eid Al-Ghadiir ni siku ya kukumbuka kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:
"Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni Neema yangu na nimeuridhia kwenu Uislam kuwa ndiyo dini" (Qur'an: 5:3).
 

Aya hii ilishuka Ghadiir Khum baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kumsimika Imam Ali bin Abi Talib (a.s) kuwa Kiongozi wa Ummah wa Kiislam, riwaya hii imepokelewa kutoka kwa Maimamu wa kizazi kitukufu cha Mtume (s.a.w.w), na ndio maana utawaona (Mashia) wanauhesabu Uimamu kuwa ni miongoni mwa "Misingini ya Dini" (Usulud-Din).

Wanachuoni wa Kisunni pia wanakubaliana kuwa Aya hii ilishuka Ghadiir Khum baada ya kusimikwa Imam Ali bin Abi Talib (a.s).

Rejea: Tarikh Dimishq ya ibn Asakir Juz. 2 Uk. 75., Manaqib Ali bin Abi Tali cha Ibn Maghazili As-Shafii Uk. 19., Tafsir ibn Kathir Juz. 2 Uk. 14.