MWALIKO.

Bismillah Taa'lah.

Tunapenda kuwakaribisha katika Sherehe ya Eid Mubahala, itakayofanyika leo siku ya J.tano tarehe 30/10/2013 Masjid Al-Ghadiir, Kigogo Post, Dar es Salaam, baada ya Swala ya Magharib. Fikisha ujumbe kwa wengine Insh'allah

"Na atakayebisha nawe katika hili baada ya ujuzi uliokujia, basi waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, ma wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu na tuiweke laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uongo." (Qur'an: 3:61)

Tarehe ishirini na nne mfungo tatu mwaka wa kumi Hijiria, ujumbe wa Kikiristo kutoka Najirani katika nchi ya Yemen, ukiongozwa na Makasisi watatu: Ahtam, Al-aaqib na Sayyid. Walikutana na Mtume (s.a.w.w) kwa majadiliano juu ya Issa (a.s) kwa kuwa Nabii Issa (a.s) alizaliwa bila baba, Wakristo wamedhani kuwa baba yake ni Mwenyezi Mungu. Mtume Mohammad (s.a.w.w) akawasomea Aya: "Hakika mfano wa Issa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam, aliumbwa kwa udongo kisha akamwambia kuwa naye akawa." Wakristo wakaendelea kushikilia itikadi yao batili, ndipo Mtume (s.a.w.w) akaamrishwa na Mwenyezi Mungu katika Aya hii kuwataka wafanye maombi ili laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uongo.