Waislamu nchini Ufaransa wamefanya maandamano ya kupinga hatua ya kubatilishwa ruhusa ujenzi wa msikiti katika mji wa Shell nchini humo. Maandamano ya wakazi hao wa Kiislamu wa mji huo yamejiri baada ya kuenea habari zinazodai kufutwa kibali cha ujenzi wa msikiti na kuwalazimu kufanya maandamano mbele ya ofisi ya baraza la mji na kutaka kufanyika uchunguzi kuhusiana na madai hayo. Wajumbe wa baraza hilo la mji waliokuwa wamekutana katika ofisi hiyo kwa ajili ya kuchunguza kadhia mbalimbali za mji huo, walikabiliana na maandamano ya Waislamu waliokuwa wamekusanyika mbele za ofisi. Aidha katika kujaribu kutuliza hali ya mambo, wajumbe hao waliwataka wajumbe wengine ambao ni Waislamu katika baraza hilo la mji kuwasilisha mapendekezo yao katika kikao kijacho. Katika kikao hicho meya wa mji huo wa Shell alitangaza kuakhirishwa mjadala wa kupatiwa Waislamu ardhi kwa ajili ya ujenzi wa msikiti hadi miezi miwili ijayo na kwamba, baraza la mji halina lengo la kufuta kikamilifu kibali cha ujenzi wa vituo vya ibada vya Waislamu. Katika miezi ya hivi karibuni, Waislamu nchini Ufaransa wamekuwa wakikabiliwa na wimbi la ubaguzi wa serikali dhidi yao.
WAISLAMU UFARANSA WAANDAMANA KUDAI MSIKITI..