ITA VYA MIAKA NANE HAVIKUWA NA MFANO KATIKA HISTORIA.


Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran, Ayatullah Muhammad Imami Kashani, amesema kuwa, hatua ya taifa la Iran ya kujihami kutakatifu kwa muda wa miaka minane katika vita vya ambavyo taifa la Iran lililazimishwa kupigana na utawala wa Saddam Hussein wa Iraq, ina athari chanya katika historia ya mwanadamu. Amesema, kujihami huko kulikofanywa na taifa la Iran kulikuwa ni harakati katika njia ya Uislamu na Mwenyezi Mungu, ambapo katika harakati hiyo, vijana shupavu wa taifa la Iran walijitolea muhanga maisha yao katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kulinda uhuru, izza, mipaka na heshima ya taifa lao. Aidha Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa mjini Tehran, amegusia hotuba iliyojaa maneno ya kimantiki iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mkutano 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko mjini New York, Marekani, na kusema kuwa, hotuba hiyo imebainisha dhulma ya madola ya kibeberu hasa Marekani dhidi ya taifa la Iran.