TANGAZO.

HAWZA IMAM JA'FAR SWAADIQ (A.S) PAMOJA NA IMAM BUKHARY ISLAMIC FOUNDATION.

Wanapenda kuwakaribisha Waislam na wasio kuwa Waislam katika Semina.

Mada: DHULMA ZINAZOFANYIWA UBINADAMU DUNIANI. MTAZAMO WA WAISLAM DHIDI YA DHULMA ULIMWENGUNI.

Semina ya kupinga dhulma inayofanywa na nchi za Kimagharibi ulimwenguni, itafanyika siku ya Jumapili 29/09/2013. Katika ukumbi wa Lamada Hoteli, Ilala kuanzia Saa 3:00 Asubuhi hadi 10:00 jioni. Kutakuwa na hotuba kutoka kwa Viongozi wa Dini mbalimbali, pia maswali na majibu yatakuwepo.

Nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani zinapanga kuishambulia Syria. Hivyo ni jukumu la kila mtu bila kujali Dini wala Madhehebu kupinga Uonevu/Mauwaji/Uvamizi dhidi ya Syria. Mwenyezi Mungu anasema katika Kitabu chake kitukufu: "Mwezi mtukufu kwa mwezi mtukufu, na vitu vitakatifu vimewekewa kisasi. Basi anae washambulieni, nanyi pia mumshambulie kwa kadiri alivyowashambulieni, na muogopeni Mwenyezi Mungu na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wamchao." (2:194)

"KILA MPENDA HAKI AJIANDAE KUHUDHURIA SEMINA."

__________________________________

Kwa maelezo zaidi piga simu:

Mohammed Mputa / 0786750004
Jamal Mackroy/ 0713888275