UZINDUZI WA KITABU UTAKAOFANYIKA MASJID AL GHADIIR, KIGOGO POST, JIJINI DAR ES SALAAM.

Tunapenda kuwakaribisha Waislam wote katika Uzinduzi wa Kitabu kiitwacho "SHIMO REFU ALILOTUMBUKIA IBN MAFUTA (KASSIM MAFUTA)", Uzinduzi huo utafanyika siku ya Ijumaa baada ya Swalatul Jumaa, tarehe 6-9-2013, Masjid Al-Ghadiir, Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, Kitabu hicho ni majibu ya kitabu kiitwacho, UYAHUDI nyuma ya pazia la AHLUL BAYT (a.s).

Makusudio makubwa ya waandishi hawa wa Kiwahhabi (Answaru Sunna) ni kupanda mbegu za chuki na utengano baina ya Waislam katika Afrika Mashariki na kwingineko, wakiwa wanatumiwa kikamilifu na maadui wa Uislam ili wahakikishe kwamba umoja wa Waislam haupatikani na kwamba hakuna hatari kwa ajili ya maslahi ya mabwana zao. Hivyo, wanatumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandika vitabu, makala, vipeperushi na Mihadhara ili kutumia uelewa mdogo wa Waislam walio wengi kwamba umoja baina ya Waislam hauwezekani na kwamba Uislam ni Uwahhab au kama wanavyojiita siku hizi ANSWARU SUNNA au SALAFII. Mgomvi wao mkubwa ni SHIA, kwa vile SHIA wanasimama imara kutetea umoja wa Waislam bila kujali itikadi zao za Kimadhehebu. Hivyo, Kimeandikwa kitabu hicho, UYAHUDI nyuma ya pazia la AHLUL BAYT (a.s) ili kuuponda USHIA. Na si USHIA tu bali na Madhehebu nyinginezo ili kuuposha Ummah huu wa Kiislam ili wasiweze kuungana na kuwa na kauli moja mbele ya maadui zao.
Kutokana na hali hiyo Mwandishi wa kitabu ameamua kutoa majibu ya kina kuhusu uzandiki wa mwandishi huyu wa Kiwahhab. Ni muhimu kwa kila Uislam kupata kopi ya kitabu hiki kwa ajili ya kujua ukweli sahihi ni upi? na sii kufuata mambo kibubusa. Fikisha ujumbe kwa watu wote, Insh'allah Mwenyezi Mungu atakulipa Kheri.