IRAN YALAANI MASHAMBULIO YA KIGAIDI NCHINI IRAQ.


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bi. Marzieh Afkham amelaani mashambulio ya hivi karibuni ya kigaidi nchini Iraq.
Akizungumza Jumatano, Afkham alisema: “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalaani jinai ambazo zinalenga kudhuru umoja wa kitaifa Iraq.”
Ameelezea matumaini yake kuwa Wairaqi chini ya uongozi wa viongozi wa kisiasa na kidini wataweza kuzima njama za magaidi wanaotaka kuvuruga uthabiti na usalama nchini humo.
Katika siku za hivi karibuni magaidi wenye mfungamano na al-Qaeda wamezidisha hujuma zao nchini Iraq kwa kuwalenga Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni. Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu 800 waliuawa nchini humo na wengine 2,000 kujeruhiwa katika mwezi uliopita wa Agosti. Chanzo cha habari
http://kiswahili.irib.ir/habari