Upotovu wa Madhehebu ya "UWAHHABI" (ANSWARU SUNNA).
Kwa yeyote anayeitaji Kitabu hiki naweza kuwasiliana nasi kwa simu
namba 0786750004,0222664158 au unaweza kufika Masjid Al-Ghadiir Kigogo
Post, jijini Dar es Salaam.
kitabu
hiki kimetafsiriwa kwa Lugha ya Kiswahili kutoka katika Lugha ya
Kingereza katika Kitabu kiitwacho (Shi’i Islam) kilichondikwa na Sheikh
Muhammad Ali Shomali na kutarjumiwa na al-Haj Ramadhani S. K.
Shemahimbo. Sisi tumekiita, Uislamu wa Shia.
Ni ukweli
usiopingika kwamba madhehebu ya Kiislamu ya Shia imekuwa ikijulikana kwa
muda mrefu kama ni madhehebu isiyoeleweka vizuri miongoni mwa Waislamu
walio wengi ulimwenguni. Hii imetokana na kukandamizwa kwa muda mrefu
wafuasi wa madhehebu hii kulikofanywa na dola zinazojiita za Kiislamu.
Kwa nini wamefanya hivyo? Historia inayo majibu ya hilo.
Waandishi wanavyuoni wengi wa sasa wamejitahidi na wanaendelea na
jitihada hiyo kuuelemisha Umma kuhusu Waislamu hawa wa Shia; na kitabu
hiki ni miongoni mwa vitabu vingi vilivyoandikwa na wanavyuoni hawa juu
ya usahihi wa madhehebu hii.
Ni muhimu kukubaliana na kuziheshimu tofauti za kila mmoja na kutambua msimamo na mtazamo wa kila mmoja.
Matatizo huja pale mtu anapolazimisha tabia, imani na mila zake zitawale wengine au kuzifisha itikadi na misimamo ya wengine.
Ni muhimu kufikiria kila aina ya maoni katika kujaribu kuamua ukweli. Uislamu kimsingi uko dhidi ya kufuata kibubusa.
Wafuasi wa madhehebu nyingine kiumakini wanaweza kuchambua mada
zilizomo katika kitabu hiki ili kujenga maoni yao wenyewe kuhusu mtazamo
mzuri wa mtu mwenyewe. Ni muhimu mtu kuelewa hoja za wale ambao
hakubaliani nao.
Inaweza ikasemwa kwamba wale ambao hawaelewi kabisa mtazamo wa maoni tofauti, hawaelewi kwa ukamilifu mtizamo wa kwao wenyewe.
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa
maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za
kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika
akili za watu.
Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya
al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya
Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan
wazungumzaji wa Kiswahili.
Tunamshukuru ndugu yetu, al-Haj R.
S. K. Shemahimbo kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki.
Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine
hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.
Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu.
Mchapishaji:
Al-Itrah Foundation
Like · · Share
Unaweza kukipata Masjid Al Ghadiir Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, Tanzania unaweza kuwasiliana nasi kupitia 0786750004