Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema leo kuwa Waislamu wako macho na kwamba yeyote atakayeanzisha vita dhidi ya Syria atafunikwa kabisa na moto wa vita hivyo.
Ayatullah Muhammad Ali Movahhedi Kermani amesema Marekani, utawala ghasibu wa Israel na waitifaki wao wamekuwa wakipiga ngoma za vita dhidi ya Syria lakini wamegundua hatari inayowakabili na ndio maana kwa sasa wameamua kutia ulimi puani. Ayatullah Kermani amesisitiza kuwa, nchi yoyote itakayoanzisha mashambulizi dhidi ya Syria iwe tayari kuungua kwenye moto wa vita hivyo. Ametahadharisha kuwa, Marekani ikijaribu kuingilia kijeshi mgogoro wa Syria itapatwa na aibu kama iliyoupata muungano wa Usovieti miaka ya huko nyuma. Khatibu wa Muda wa Sala ya Ijuma hapa Tehran ameukumbusha Umma wa Kiislamu kwamba, Utawala haramu wa Israel ndio chanzo cha matatizo katika eneo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika na kuwataka Waislamu wajiepushe na utawala huo wa Kizayuni. Huku hayo yakijiri, Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa, Bashar Ja'afari amesema kuwa, Rais wa nchi yake, Bashar Assad ametoa agizo la kusainiwa mkataba wa WCW unaopinga usambazaji na utumiaji wa silaha za sumu. Itachukua muda kabla ya nchi hiyo kuwa mwanachama ingawa weledi wa mambo wanasema hiyo ni hatua moja mbele kwa Syria kuangamiza silaha za kemikali na kwamba nchi zingine zinapaswa kufuata mkondo huo.
JESHI LA ISRAEL LAWAZUIA WAPALESTINA KUINGIA MASJIDUL AQSA.
Jeshi la utawala haramu wa Israel limekuwa likiwazuia watoto wa Kipalestina kuingia Masjidul Aqsa katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.
Gazeti la Kizayuni la Maariv limeandika kwenye toleo lake la Ijumaa kuwa, hatua hiyo ya jeshi inatokana na hoja iliyowasilishwa na wabunge wa mrengo wa kulia katika bunge la utawala huo ghasibu. Wanajeshi wa Israel pia wamewazuia vijana wa Kipalestina wa kati ya umri wa miaka 10 hadi 30 kuingia katika msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.
Utawala ghasibu wa Israel umekuwa ukijaribu kufuta utambulisho wa Kiislamu katika mji wa Quds na vilevile umejaribu haribu msikiti wa al-Aqsa kwa kuchimba mashimu kwenye misingi yake licha ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kuutangaza kuwa eneo la kihistoria. Chanzo cha habari http://kiswahili.irib.ir/habari/habari/item/34657-jeshi-la-israel-lawazuia-wapalestina-kuingia-masjidul-aqsa. Chanzo cha habari
http://kiswahili.irib.ir/habari