UMOJA NA MSHIKAMANO HAUFIKIWI KWA NARA BALI UTAFIKIWA KWA VITENDO.


Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Dkt. Hassan Rohani amesema umoja na mshikamano haufikiwi kwa nara bali utafikiwa kwa vitendo.

Dkt. Rohani ameyasema hayo leo mchana mjini Tehran katika sherehe za kumuaga waziri wa zamani na kumkaribisha waziri mpya wa mambo ya ndani.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema serikali mpya ambayo kaulimbiu yake ni ‘Tadbiri na Matumaini’ hakupaswi kuwepo na ubaguzi wa kimadhehebu, kikaumu  na makundi mengine ya walio wachache. Aidha amesema misimamo ya kufurutu mipaka ni hatari kwa maslahi ya taifa na kuongeza kuwa serikali yake haipendelei mrengo wowote wa kisiasa nchini. Rohani ameendelea kusema kwamba misimamo ya kufurutu mipaka si tu kuwa ni hatari kwa maslahi ya taifa bali hata kwa Umma wa Kiislamu na jamii ya kimataifa.

Rohani ametoa wito kwa waziri mpya wa mambo ya ndani Bw. Abdolreza Rahmani Fazli kuwapa nyadhifa watu wa makundi ya waliowachache na wanawake. Rohani amesema kile ambacho anazingatia katika uteuzi ni kufungamana na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, uwezo wa kikazi, uaminifu na moyo wa kujitolea.