TAARIFA KWA WAUMINI.

Bismillah Rahmanir Rahiim

Kamati ya kutoa taarifa ya Mwezi imewasiliana na watu wa sehemu zote wanazodai Mawahhab (ANSWARU SUNNA) kuwa wameuona Mwezi, watu wa miji hiyo wamekanusha kuonekana kwa Mwezi katika sehemu hizo kwa hiyo kesho tunafunga kukamilisha thelathini (30), Insh'allah Mwenyezi Mungu (s.w) akipenda Swala ya Idd itaswaliwa siku ya Ijumaa Masjid Ghadiir Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, kukifuatiwa na Salamu za Idd kutoka kwa Viongozi mbalimbali, pia watu wote tutajumuika katika chakula cha mchana pamoja kwa ajili ya kuimalisha umoja na mshikamano baina yetu. Fikisha ujumbe kwa mwengine Insh'allah

Suala la kufunga na kufungua Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikifuatiwa na Sikukuu za Idd El-fitri na Idd El-adh'ha, limekuwa likitumiwa na kundi la Mawahhab (ANSWARU SUNNA) kujenga utengano baina ya Waumini kiasi cha kuwaita makafiri  wale wasiofuata maoni yao ya kujitenga na kuswali Idd wakati Waislamu wengine bado wamo ndani ya Swaumu.

Mawahhab (ANSWARU SUNNA) wanadai kufunga na kufungua kwa kufuata tangazo la Serikali ya Saudi Arabia kana kwamba wao ni wakazi wa nchi hiyo, na kwamba wanapofunga wao lazima ulimwengu mzima ufanye hivyo. Hakuna mafundisho ya Kiislamu yanayoipa Serikali ya Saudi Arabia haki ya kuamua kutangaza kuandama mwezi bila kuonekanwa mwezi wenyewe wala hakuna mafundisho yanayowataka Waislamu wafunge au kufungua kwa tangazo la Serikali ya Saudia.

Imepokewa hadithi kutoka kwa Ibn Umar (ra) kuwa amesema:
Amesema Mtume (s.a.w): "Msifunge mpaka mtakapouona mwezi, wala msifungue mpaka muuone, ukifunikwa na wingu ukadirieni (kwa kutimiza siku thelathini)" (Imepokewa na Bukhar na Muslim katika vitabu vyao sahihi)

Hiya ndio mafundisho sahihi ya Uislamu yanayotokana na Maswahaba kutoka kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w).