SWALA YA EID AL FITRI IMESWALIWA MASJID AL GHADIIR KIGOGO POST, JIJINI DAR ES SALAAM.

Maulana Sheikh Hemed Jalala,
amewataka Waumini wa Madhihabu ya Ahlul-Bayt(a.s), kushilikiana na Makao Makuu yao (Tanzania Ithna Ashariyyah Community), amesema kuwa laiti kama Wafuasi wa Madhihabu ya Ahlul-Bayt (a.s) wataonyesha ushirikiano baina yao na Makao Makuu watapiga hatua zaidi katika kufikisha ujumbe wa Ahlul-Bayt (a.s), kwa maana  Madhihabu ya Ahlul-Bayt (a.s), yanakubalika na maumbile ya Mwanadamu kwa hiyo huwezi kueleza Madhihabu ya Ahlul-Bayt (a.s), sehemu ukapata upinzani zaidi ya kuungwa mkono hasilimia mia, hivyo amesisitiza kuwa wa moja baina yao hili waweze kufikia lengo kuu, amesema hayo katika swala ya Eid Al Fitri, iliyoswaliwa leo Masjid Ghadiir Kigogo Post, jijini Der es Salaam.

Mudir wa Hawzat Al-Imam Swaadiq (a.s) iliyopo Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, akitoa hotuba kwa Ummah wa Kiislam baada ya Swala ya Eid Al Fitri, iliyoswaliwa leo Masjid Al Ghadiir Kigogo Post.
 Waumini wa Kiislam wakiwa Masjid Ghadiir Kigogo Post, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Swala ya Eid Al Fitri.