Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, matukio ya magharibi mwa Asia hususan Palestina na yale ya kaskazini mwa Afrika yanatia wasi wasi mno. Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo katika hotuba ya Sala ya Eid ul Fitri mjini Tehran na kusisitiza kwamba, matukio ya Palestina ya kukaliwa kwa mabavu ardhi za Wapalestina, dhulma wanayotendewa na ukandamizaji wanaofanyiwa wananchi hao kila leo ni mambo yanayotia uchungu. Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Kiislamu amesema, kubomolewa nyumba za Wapalestina, kutenganishwa watoto na wazazi wao na kuongezeka wafungwa wa Kipalestina katika magereza ya Wazayuni ni miongoni mwa masaibu na misiba ya Wapalestina; hata hivyo chungu zaidi ni himaya ya kila upande ya madola ya Magharibi kwa utawala haramu wa Israel unaotenda jinai kila leo dhidi ya Wapalestina. Ayatullah Khamenei amesema, madola yanayodai kuwa watetezi wa haki za binadamu yamekuwa yakiunga mkono jinai za Wazayuni makatili. Kiongozi Muadhamu ameashiria matukio ya sasa ya Misri na kusema kwamba, kila siku uwezekano wa kutokea vita vya ndani nchini humo umekuwa ukiongezeka. Ameyaonya madola ya kibeberu na kuyataka yaache kuingilia masuala ya ndani ya Misri; kwani hatua yao hiyo ni kwa madhara kwa taifa la Misri.
MATUKIO YA PALESTINA YANATIA UCHUNGU MNO.