SABABU ZINAZO WAFANYA VIJANA KUSHIKAMANA NA DINI.


Kuna sababu nyingi katika hali ya vijana kukubali kuingia katika dini:-

1- Katika hatua ya ujana ufahamu wa mwanadamu unapopevuka na fikra zake zinafunguka katika maisha na kumjia mbele ya
ke maswali yanayofaa, maumbile yake yanauliza na kuihamasisha akili yake, na kutokana na kutafakari kwake na udadisi wake wa kutafiti yanayomzunguka miongoni mwa mambo na hali yanajitokeza maswali mengi, na kwa kuwa dini inampa majibu yaliyo wazi yanayokubaliana pamoja na maumbile na yanayoafikiana pamoja na hali ya kawaida ya akili basi kijana anakuta dini ndio chaguo lake na ngome yake anayoikimbilia na kumpa matumaini ya kinafsi na utulivu na kifikira.
Na inapokosekana fursa ya kujua dini na uelewa wa misingi yake na mafunzo yake basi anaweza kuishi katika faragha ya kifikra na kinafsi inayomsababishia hofu nyingi na mkanganyiko, na anakuwa ni muathirika wa mielekeo ya kimakosa yenye kupetuka, kuanzia hapa umekuja msisitizo wa dini juu kuwajali chipukizi na vijana kupitia familia zao na wenye kufahamu miongoni mwa wanajamii ili kuhifadhi kizazi cha vijana kutokana na faragha na upotevu.
Imam Ali (a.s) anasema: "Hakika moyo wa kijana ni kama ardhi isiyo na kitu na kila kinachopandwa humo inakikubali."
Rejea: Al-Musawiy: As-Sharifu ar-Ridhaa katika Nahjul-Balaghah, kitabu cha (hotuba) ya 31.

Na kutoka kwa Imam Ja'far As-Saadiq (.a.s) anasema: "Wawahini vijana wenu kwa mazungumzo kabla hawajawahiwa na waovu miongoni mwa makundi maovu."
Rejea: Al-kulayn: Muhammad bin Yaaqub katika Furu'ul-Kaafiy J. 6 Uk. 47.

2- Kijana anakuwa mwepesi wa hisia, msafi wa fikra na nia, hivyo anahisi kwa kina nukta za udhaifu na mianya katika uhalisia wa jamii anayoishi, na kwa sababu anafikiri katika kujenga mustakabali wake na maisha yake ndani ya jamii hii, hakika matatizo na taabu zilizopo zinamuudhi na kumfanya ahisi huzuni juu ya mustakabali wake na anaweza kuona kwamba ufahamu wake na matarajio yake yanakwazwa katika nyanja ya kujifunza au kazi au kujenga familia na kupanga mambo ya maisha kwa sababu ya baadhi ya matatizo yaliyopo, ambapo yanamfanya atafute mategemeo ya ukombozi na ataona humo mustakabali ulio bora.

Dini inakuza kwa mwanadamu roho ya ufahamu bora na inatia moyo wa kukabiliana na matatizo ya mazingira anayoishinayo mtu, na kutonyenyekea katika ufisadi wake na matatizo yake, na kumshajiisha juu ya kazi kwa ajili ya kutengeneza na kubadilisha, na haya ndio mambo ambayo nyoyo za vijana zinayatarajia na zinaafikiana nayo.
Vijana wa Makka na Madina walimwitikia Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakaingia katika Uislam kwa sababu wao waliona humo ujumbe wa mabadiliko na mapinduzi ya ukombozi kutokana na ujahili, Shirki na Ufisadi wa kijamii. Na viajana wa Kiislam katika zana hii wanakubaliana na Harakati za Kiislam kwa sababu ya yale wanayoyaona miongoni mwa Machungu ya hali ya Ummah wao, ikiwemo kurudi nyuma kimaendeleo, utawala wa maadui, hali ya ukandamizaji na ufisadi ulioenea, hivyo wanakimbilia kwenye Uislam kama meli ya uwokozi na ni mradi wa ukombozi na urekebishaji.

3- Ni muda sasa yamerundikana makosa na kupatikana upotovu hata katika jamii nzuri, hivyo jamii zinahitaji kutikiswa na harakati za mageuzi ili zibadilike kupitia ratiba ya maisha na zivuke vihunzi vya makosa na ubaya, lakini kazi hii inaweza kuwa ngumu kwa kizazi cha wakubwa, kwani wao wameshazoea hali ya maisha, njia zake na mbinu zake, na wao wanaogopa nyongeza ya mabadiliko, na aghlabu hawamiliki moyo wa mapambano na matumaini.
Ama vijana mafungamano yao na hali iliyopo ni mafungamano mapya na finyu, na moyo wao wa kufungamana na hali iliyopo ni dhaifu ambapo hauyaridhishi matumaini yao, na hivyo haraka sana hali hiyo inawasukuma vijana katika mapambano na kuvamia wasiyoyajua kwa kutafuta kilicho bora. Na dini kwa uhakika wa dhana yake na mafunzo yake, ni wito wa daima wenye kutengeneza na kuhimiza juu ya kubadilisha kiovu na kukubali kizuri katika nyanja yoyote miongoni mwa nyanja za maisha. Na hivyo ndio alama inayowavutia vijana na kuwahifadhi katika dini.