Rais Hassan Rohani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameapishwa rasmi leo Jumapili katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, yaani Bunge la Iran. Baada ya kuapishwa, Dk Hassan Rohani amelihutubia Bunge na kusema kuwa, moja ya vipaumbele vikuu vya serikali mpya ya Iran itakuwa ni kuleta maelewano zaidi kati ya Iran na nchi nyingine duniani sambamba na kutia nguvu usalama wa ndani na nje ya mipaka ya Iran. Amesema, serikali mpya ya Iran itafanya juhudi zake zote kuhakikisha kuwa katika miamala yake ya kimataifa kunapatikana maelewano zaidi baina ya Iran na nchi nyingine za dunia pamoja na kulinda usalama na amani ya ndani ndani na nje ya Iran. Wakati huo huo lakini amesema kuwa, si jambo linalowezekana kuweko uwazi na kuonyesha nia njema kwa upande mmoja akisisitiza kuwa, kamwe Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi kuanzisha vita dhidi ya nchi nyingine na siku zote imekuwa ikielekeza juhudi zake katika kupambana na watu wanaopiga ngoma ya vita duniani. Vile vile amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaamini kuwa, mfumo wa kisiasa wa kila nchi unategemea maamuzi ya wananchi wa nchi hiyo na inapinga kabisa utumiaji mabavu katika maamuzi ya nchi. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/habari/iran/item/33804-rohani-aapishwa,-asisitizia-uhusiano-mwema-na-nchi-nyingine
ROHANI AAPISHWA, ASISITIZIA UHUSIANO MWEMA.