Sherehe za kuapishwa Dakta Hassan Rohani, Rais mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimefanyika leo alasiri tarehe 4 Agosti katika ukumbi wa bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Shughuli rasmi za rais huyo wa kipindi cha 11 cha urais wa Iran, zilianza jana baada ya kuidhinishwa na Kiongozi Muadhamu kuwa rais mpya wa Iran na rais huyo kuapishwa leo mbele ya bunge. Kwa mujibu wa kifungu nambari 9 kipengee 110 cha katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kipindi cha miaka minne cha rais, huanza kwa kuidhinishwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Dakta Hassan Rohani ameapishwa leo katika jengo la Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani bunge la Iran, mbele ya viongozi na wageni rasmi kutoka zaidi ya nchi 60 za mabara matano ya dunia. Kwa muktadha huo, kipindi cha urais wa Dakta Hassan Rohani ambaye kaulimbiu yake ni kutatua matatizo ya wananchi, kujenga imani kwa wananchi na kuwa na msimamo wa wastani kuhusiana na siasa za nje, kilianza rasmi hapo jana Jumamosi na rais aliyemtangulia, Dakta Mahmoud Ahmadinejad alimkabidhi rasmi ufunguo wa ofisi za Rais hiyo hiyo jana. Kwa upande mwingine kuhudhuria viongozi na wageni kutoka nchi mbalimbali za dunia katika sherehe za kuapishwa Rais Hassan Rohani, kunatajwa na duru za kisiasa na kihabari kuwa ni ishara ya kupanuliwa zaidi uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kieneo na kimataifa. Kuhusiana na suala hilo, Shirika la Habari la Associated Press limeripoti kutoka Washington kuwa, huku rais mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akijiandaa kuanza rasmi shughuli za kuliongoza taifa, Marekani inafanya njama za kuiwekea vikwazo vingine nchi ya Iran. Kwa mujibu wa shirika hilo la Associated Press, siku ya Jumamosi maseneta 76 wa Marekani walimuandikia barua Rais Barack Obama wa Marekani, wakimtaka kushadidisha zaidi vikwazo dhidi ya Tehran ili kwa njia hiyo na kwa mujibu wa fikra za maseneta hao, waweze kuilazimisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kupunguza shughuli zake za nyuklia zenye malengo ya amani. Katika barua hiyo pia viongozi hao walimtaka Obama kulifanyia kazi pendekezo la kijeshi dhidi ya Iran, sambamba na kufungua mlango wa kidiplomasia na taifa hili. Kwa mujibu wa maseneta waliotia saini barua hiyo, hivi sasa Iran inaendelea kwa kiwango cha juu kabisa katika kuweka mashinepewa (Centrifuge) kwa ajili ya shughuli za nyuklia. Madai ya maseneta hao, yanatolewa katika hali ambayo, miradi ya nyuklia ya Iran, haijakwenda kinyume hata kidogo na makubaliano ya kuzuia utengenezaji na usambazaji wa silaha za nyuklia NPT. Itakumbukwa kuwa, tarehe 31 Julai, Baraza la Kongresi la nchi hiyo, lilipasisha mpango wa kushadidisha vikwazo vipya vya mafuta dhidi ya taifa hili. Kwa mujibu wa muswada huo, Marekani inapanga kuzishinikiza nchi zinazonunua mafuta ya Iran ili zipunguze mapipa milioni moja kila siku katika kiwango cha mafuta yao zinayonunua kutoka Iran. Hii ni katika hali ambayo hivi karibuni pia, maseneta kadhaa wa nchi hiyo kwa kushirikiana na wajumbe wa baraza hilo hilo, walimuandikia barua nyingine rais wa Marekani wakimtaka kufanya mazungumzo ya kweli na taifa hili hasa baada ya kuchaguliwa Dakta Hassan Rohani. Misimamo hiyo ya kupingana inawafanya weledi wa mambo kutia shaka misimamo ya Marekani. Baadhi ya weledi wa masuala ya kisiasa wanawakosoa viongozi wa Washington kuwa, hawakuweza hata kusubiri kuona kwamba, ni hatua gani zitachukuliwa na rais mpya wa Iran kuhusiana na kadhia ya nyuklia ya nchi hii. Hata hivyo, misimamo hiyo ya kindumilakuwili ya Marekani, haikuwashangaza wengi. Hii ni kwa sababu, kabla ya hapo taifa hilo la kibeberu, limekuwa likitangaza kutaka kufanya mazungumzo na taifa hili huku likishadidisha mashinikizo na vikwazo vya kisiasa na kiuchumi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, misimamo ambayo imekuwa ikiongeza mivutano baina ya Iran na nchi za Ulaya. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/uchambuzi/item/33797-duru-mpya-ya-urais-wa-jamhuri-ya-kiislamu-ya-iran-na-misimamo-hasi-ya-marekani
DURU MPYA YA URAIS WA JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN NA MISIMAMO HASI YA MAREKANI.