Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameelezea kusikitishwa na hatua ya nchi moja ya kuzuia ndege iliyokuwa imembeba Rais wa Sudan aliyekuwa anaelekea mjini Tehran kwa ziara rasmi.
Sayyid Abbas Araqchi amesema kuwa, Ubalozi wa Sudan Tehran umeitaarifu Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kuwa, nchi moja imekataa anga yake kutumiwa na ndege iliyokuwa imembeba Rais Omar Al Bashie wa Sudan ambaye alikuwa anaenda mjini Tehran kushiriki kwenye sherehe za kuapishwa Dk. Hassan Rohani kuwa Rais wa Saba wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, Saudi Arabia imeikatalia ndege iliyokuwa imembeba Rais Omar al Bashir kupita kwenye anga yake na ndege hiyo kulazimika kurudi mjini Khartoum, Sudan.