Kufuatia kuanza kile kinachojulikana kama mazungumzo ya mapatano baina ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Mamlaka ya Ndani ya Palestina, kumeanza kushuhudiwa wimbi jipya la njama za Israel lenye lengo la kupotosha kikamilifu haki za Wapalestina hususan hatua yake ya kukataa kuwaachilia huru mateka wote wa Kipalestina. Utawala wa Kizayuni umekubali kuwaachia huru Wapalestina wachache tu tena katika awamu nne. Kuhusiana na suala hilo, Saeb Uraiqat, kiongozi wa timu ya mazungumzo ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina alisema Jumamosi ya jana kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel umekataa kuwaachia kwa mara moja mateka wa siku nyingi wa Kipalestina na badala yake umesema kuwa, utawaachilia huru mateka hao kwa awamu nne. Kwa mujibu wa ripoti ni kuwa, kundi la kwanza la mateka hao linalojumuisha mateka 26 litaachiliwa huru tarehe 13 ya mwezi huu wa Agosti. Idadi ya mateka wa Kipalestina ambao baraza la mawaziri la Israel limekubali kuwaachia huru ni 104 tu kati ya mateka zaidi ya elfu tano wa Kipalestina. Wataalamu wa mambo wanaamini kwamba, hatua hiyo ni njama mpya ya utawala huo ya kutaka kujionesha kwamba, unapenda amani. Hii ni katika hali ambayo, hatua hiyo haina lengo jingine ghairi ya kuzidi kuzikanyaga haki za wananchi madhulumu wa Palestina na wakati huo huo kuandaa mazingira ya kuendelea kuishikilia mateka idadi kubwa ya Wapalestina. Hapana shaka kuwa, hatua ya Mamlaka ya Ndani wa Palestina ya kutaka kufanya mapatano na utawala wa Kizayuni wa Israel imekuwa ikiupa kiburi utawala huo ghasibu cha kuendeleza hatua zake zisizo za kibinaadamu likiwemo suala la kukwepa kuwaachilia huru mateka wote wa Kipalestina. Hatua ya Marekani nayo ya kunyamazia kimya masuala kama ya hali ya mateka na wakimbizi wa Kipalestina katika mpango wake mpya wa kuhuisha mazungumzo eti ya mapatano baina ya Israel na Mamlaka ya Ndani ya Palestina maana yake ni kuipa idhini Tel Aviv ya kushadidisha jinai zake dhidi ya Wapalestina. Katika mazingira kama haya, utawala wa Kizayuni ukiwa na lengo la kupotosha suala la kuwaachilia huru mateka wote wa Kipalestina unafuatilia suala la kuwauwa kwa umati Wapalestina hao. Matamshi ya hivi karibuni ya Waziri wa Uchumi wa Israel yanaweza kutathminiwa katika kalibu hii. Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, utendaji wa Israel kuhusiana na suala la mateka wa Kipalestina na misimamo ya viongozi wa utawala huo katika miezi ya hivi karibuni ni mambo yanayobainisha juu ya kuweko njama za umwagaji damu za Wazayuni dhidi ya mateka wa Kipalestina. Hatupasi kusahau nukta hii pia kwamba, kigugumizi na hatua za kusitasita za jamii ya kimataifa kuhusiana na mateka wa Kipalestina, nazo zinazidi kuzifanya roho za Wapalestina zizidi kukabiliwa na hatari. Habari kutoka http://kiswahili.irib.ir/uchambuzi/item/33791-njama-mpya-za-utawala-wa-kizayuni-kuhusu-mateka-wa-kipalestina
NJAMA MPYA ZA UTAWALA WA KIZAYUNI KUHUSU MATEKA WA KIPALESTINA.