Bunge la Uingereza kukataa na kupinga vikali Uingereza kushiriki katika vita dhidi ya Syria, baada ya uamuzi huo Marekani kushikwa na gutwaa na kushindwa la kufanya na kutafuta wataomuunga mkono badala ya Uingereza, hapo kabla Marekani na Uingereza walitanga kuivamia Syria kijeshi kwa madai ya kutumia serikali ya Syria silaha za kamikali.
Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Marekani baada ya jitihada muda mrefu kufeli katika uamuzi wake wa kuvamia Syria kijeshi, Uingereza ni moja kati ya nchi zilizokuwa zikiunga mkono Marekani imejitowa katika fikra za kuvamia Syria baada ya Bunge la nchi hiyo kukataa kuingilia na kuvamia Syri kijeshi na kutaka kutafuta njia mbadala ambayo ni kidiplomasia.
Baada ya uamuzi huo nchi nyingi zilishuhudia maandamno makubwa na mamia ya watu kuandamana dhidi ya vita ya Syria, Uingereza waliandama wananchi kupinga kuingilia nchi yao katika mambo ya Syria.
Marekani nako kulishuhudia maandamano makubwa ya kupnga nchi yao kuvamia Syria kivita kwa madai ya kutumia serikali ya Syria silaha za kemikali dhidi ya wananchi wake, na kueleza hiyo ni njia nyengine ya kutaka kuharibu hali ya usalam nchini Syria kama walivyofanya Iraq kwa madai ya kuwa serikali ya Iraq ni silaha za Nyuklia.
Uturuki nako mamia ya wananchi waliandamana kwenye kambi ya jeshi ilokuwepo mpakani mwa Syria na Uturuki kuitaka nchi yao kutotumia ardhi ya dhidi ya Syria na kuitaka nchi kujiepusha mbali na fitina hizo za Marekani.
Mazayuni walivyokuwa na uwoga juzi walitangaza kuwa mnamo siku ya Alkhamisi (ilopita) Marekani ndio imepangilia kuvamia Syria, na kutangazi wananchi wa Israel kuchukua mask za Nyuklia kama ikitokea vita Syria itavamia Israel kwa silaha za kemikali.
La ajabu ni kwamba uamuzi wa kuvamia Syria Umoja wa Mataifa umepinga vikali kutokana na kutopatikana na ushahidi matumizi ya silaha za kemikali, na kueleza madai ya Marekani hayana nafasi kwani kila sehemu ilotumiwa silaha ya kemikali athari zake hubaki hadi wiki mbili, kwa matiki hii madai ya Marekani kuwa serikali ya Syria ilichelewa kuruhusu wakaguzi wa Umoja wa Mataifa sio kweli waliruhusiwa ndani ya muda muafaka.
JUMUIYA YA KIMATAIFA YA AHLUL BAYT (A.S) YAONYA VITA DHIDI YA SYRIA.
Ubepari wa Marekani, Uingereza na Mayahudi umefikia mahala huwezi kustahamilika kwa kutaka kumwaga damu, hatua ya uvamizi wa kijeshi dhidi ya Syria ni hatua ya hatari, bila shaka uchukuwaji wa hatua hiyo utasababisha kuharibika hali ya mashariki ya kati na kuziathiri nchi za jirani.
Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Katika kuendeleza vita baridi dhidi ya Syria nchi za Magharibi na za Kiarabu kutangaza vita dhidi ya Syria kwa madai kuwa serikali ya Syria imetumia silaha za kemikali dhidi ya wananchi wake, Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt(as) kulingana na madai hayo na kutanga za vita dhidi ya Syria ilituwa ujumbe na onyo dhidi ya Marekani na washiriki wake na kueleza kuwa hatima ya uamuzi huo ni kujutia kwa athari mbaya zitakazotokea hapo baadae.
Ujumbe kamili ni kama ufuatavyo:
بسم الله الرحمن الرحیم
Mzozo wa Syria ambao kwa sasa imekuwa kama karata ya nchi za kimaghari, Mayahudi na Mawahabi kwa madai ya kuwa hali ya Syria ni mbaya, la kusikitisha ni kwamba kila siku huonyesha kuwa hali ni mbaya, lengo la maneno hayo ni madai kua wananchi wa Syria wahitaji kuwa huru na wataka demokrasia na kutaka kuficha na kuvuta picha mzima ya Muqawama (msimamo wa wananchi) na kutaka kuletz vurugu ndani ya nchi kama walivyofanya nchi zingine, hawakuridha kwa hayo bali walikabidhi waasi silaha za kemikali kwa matumizi dhidi ya wananchi na kudai kuwa serikali ya Syria ndio watumia silaha hizo.
Kwa hali mashariki ya hitaji subira na utulivu hadi hali kuwa shwari, ubepari wa Marekani, Uingereza na Mayahudi umefikia mahala huwezi kustahamilika kwa kutaka kumwaga damu, hatua ya uvamizi wa kijeshi dhidi ya Syria ni hatua ya hatari, bila shaka uchukuwaji wa hatua hiyo utasababisha kuharibika hali ya mashariki ya kati na kuziathiri nchi za jirani, kutokana na uamuzi wa Marekani kuvamia Syria Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Sayyid Ally Khamenei alisema: Kuingilia Marekani katika mzozo wa Syria hatoona kheri na asitarajii kuwa matunda yake yatakuwa mazuri.
Aidha kuvamia Marekani kijeshi Syria kusaidiwa na washiriki wake na nchi za mashariki ya kati ni madhara kwa Israel mtoto wa haramu wa Marekani na ndio itakuwa mwisho wa Mazayuni na pesa na Qarun ambazo ni pesa na Petroli za Waarabu hazitosaidia chochote.
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul bayt(as) pamoja na wachambuzi wa siasa waitakidi kuwa njia ya utatuzi wa mzozo wa Syria ni njia ya maongezi tu na sio kuvamia kijeshi, kuchukuliwa silaha zote zilokuwepo mikononi mwa waasi na magaidi wa Syria, hiyo ndio njia pekee ya utatuzi wa mzozo wa Syria.
Ujumbe kwa nchi wanazohami waasi na kuwapa silaha waasi hao wao ndio waandalizi wa waanzilishi wa vita hiyo na wao ndio waandaa umwagaji wa damu za watu wasokuwa na hatia, twatowa onyo kwa wanaohami waasi hao hatima yao itakuwa mbaya.
Wapenzi, wahami, taasisi za kuhami haki za binadamu na wapendao uhuru ulimwenguni wapinga vikali uamuzi huo na kueleza uamuzi upo dhidi ya haki za binadamu, msimamo dhidi ya vita na kuonyesha Jumuiya za Kimataifa kuwa mambo yanayofanywa na Marekani na Israel ni kinyume na kanuni za Kimataifa na wananchi wawe pamoja na Muqawama (msimamo) na kutoruhusu waasi na Matafiki (Mawahabi) wakishiriana na Marekani kuharibu nchi yao, kumwagika barabarani kupinga hatua dhidi ya Uislamu ambayo Marekani adhamiria kuichukua.
Twaitakidi vita dhidi ya Syria ni njama za Israel na Marekani kwa kutaka kudhoofisha msimamo wa Waislamu na Uislamu kwa kuhami upinzani (waasi) kipesa kwa lengo la kupindua serikali ya Syria.
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt(as) ni Jumuiya ya Kimataifa unayohami haki za wananchi na kuwataka Waisl,i wote duniani kuwa pamoja na Waislamu wenzao kuwa kinyume na Makafiri ambao wapo dhidi ya Uislamu.
Jumuiya ilokuwa huru iso mili upande wowote ule lazima ipinge vikali uamuzi huo, lazima tujifunze na tuwe namazingatio katika visa kama kisa cha Firauni, na nguvu za Qarun, nguvu za Qarun ni Petroli ya waarabu ambayo ndio itakuwa silaha dhidi yao hii ndio tasturi ya Allah, Allah asema:
" وَلاَ تَرْكَنُواْ إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُواْ فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللّهِ مِنْ أَوْلِيَاء ثُمَّ لاَ تنصرون". (سوره هود ـ 113)
“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” Qurani 11/113
Aidha allah akieleza hatima na mwisho wa viongozi hao akisema:
" فَخَسَفْنَا بِهِ وَبدَارِهِ الْأَرْضَ فَمَا كَانَ لَهُ مِنْ فِئَةٍ يَنْصُرُونَهُ مِنْ دُونِ اللَّهِ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُنْتَصِرِين". (قصص ـ 81)
“Basi tukamdidimiza yeye na nyumba yake katika ardhi; wala halikuwepo kundi lolote la kumnusuru kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa wanao jitetea.”Qurani 28/81
رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَومِ الکَافرِين
والسلام علی عباد الله الصالحین
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt(as)
31/august/2013