DR. HASSAN RUHANI KUMPOKEA RASMI MFALME WA OMANI.

Rais wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran leo adhuhuri alimpokea rasmi mfalme wa Omani katika mji mkuu wa Tehran.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Hujatul Islam walmuslimin Dr.Hasan Ruhani rais wa Jamuhuri ya Kiislamu wa Iran leo adhuhuri alimpokea rasmi Sultan Qabus mfalme wa Omani katika mji mkuu wa Tehran.

Katika mapokezi rasmi hayo kulisomwa nyimbo za nchi mbili hizo kisha kupelekwa sehemu husika.

Safari hii inalenga kuimarisha uhusiano mzuri wa nchi mbili hizo na ujirani wema na kusaini baadhi ya mikataba.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alikutana na Sultani Qaboos bin Said, Mfalme wa Oman. Katika mkutano huo Ayatullah Khamenei aliashiria uhusiano mzuri na wa kirafiki uliopo kati ya Iran na Oman na kumbukumbu nzuri waliyonayo wananchi wa Iran kwa nchi na serikali ya Oman na akasema: "Kuna fursa kadhaa za kustawisha zaidi uhusiano wa nchi mbili katika nyanja mbalimbali hususan katika sekta ya mafuta."

Ayatullah Khamenei ameitaja nchiya Oman kuwa ni jirani mwema na wa kweli kwa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran naakasema kuhusiana na masuala ya eneo kuwa, hivi sasa eneo linakabiliwa na hali
nyeti na tete ambayo inahitajia mashauriano zaidi baina ya nchi mbili.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, eneo linakabiliwa na hatari ya kutumbukia kwenye mgogoro na akaongeza kwamba chanzo hasa cha hali iliyopo hivi sasa katika eneo ni
uingiliaji wa namna mbalimbali unaofanywa kutoka nje ya eneo hili.

Ayatullah Khamenei amesema, moja ya masuala hatari katika eneo ni kuingizwa masuala ya kidini, kimapote na kimadhehebu katika hitilafu za kisiasa baina ya nchi, na akafafanua kwa kusema:
"Kwa masikitiko ni kuwa kutokana na uungaji mkono wa baadhi ya nchi za eneolimeanzishwa kundi la ukufurishaji ambalo lina ugomvi na makundi yote yaWaislamu, hata hivyo wale wanaoliunga mkono kundi hili wanapaswa wajue kwamba moto huu utakuja kuwatambalia na wao pia."

Alisisitiza pia kuhusu tishio la utawala wa Kizayuni kwa kueleza kwamba utawala huo ni tishio la kudumu katika eneo na unaungwa mkono kwa kila hali na Marekani, na akaongezea kwa kusema:
"Kutokana na kuwa na maghala yaliyosheheni silaha hatari mno za mauaji ya halaiki, utawala harabu wa Kizayuni ni tishio kubwa kwa eneo."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa eneo linahitajia amani kwa wote, na njia pekee ya kuweza kulifikia lengo hilo muhimu ni kutangazwa kwa maana halisi marufuku ya
silaha za mauaji ya umati katika eneo hili.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Rais Hassan Rohani, Sultani Qaboos alibainisha furaha kubwa aliyokuwa nayo kwa kukutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na akasema,
uhusiano wa Iran na Oman ni mzuri sana kutokana na mafungamano ya kihistoria na kiutamaduni yaliyopo baina ya nchi mbili. Aliongeza kuwa katika mazungumzo aliyofanya na Rais wa Iran walijadili njia za kustawisha zaidi uhusiano katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na upitishaji bidhaa hususan katika
sekta ya gesi.

Aliunga mkono pia maneno ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu hali nyeti na tete
inayotawala katika eneo na tishio la utawala wa Kizayuni, na akasema: Ili kuondokana na hali iliyopo hivi sasa kuna haja ya kuzingatiwa maslahi ya wananchi wa eneo pamoja na kuwepo ushirikiano kati ya nchi za eneo.

Ayatullah Khamenei ameitaja nchi ya Oman kuwa ni jirani mwema na wa kweli kwa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran na akasema kuhusiana na masuala ya eneo kuwa, hivi sasa eneo linakabiliwa na hali
nyeti na tete ambayo inahitajia mashauriano zaidi baina ya nchi mbili.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, eneo linakabiliwa na hatari ya kutumbukia kwenye mgogoro na akaongeza kwamba chanzo hasa cha hali iliyopo hivi sasa katika eneo ni
uingiliaji wa namna mbalimbali unaofanywa kutoka nje ya eneo hili.

Ayatullah Khamenei amesema, moja ya masuala hatari katika eneo ni kuingizwa masuala ya kidini, kimapote na kimadhehebu katika hitilafu za kisiasa baina ya nchi, na akafafanua kwa kusema:
"Kwa masikitiko ni kuwa kutokana na uungaji mkono wa baadhi ya nchi za eneo limeanzishwa kundi la ukufurishaji ambalo lina ugomvi na makundi yote ya Waislamu, hata hivyo wale wanaoliunga mkono kundi hili wanapaswa wajue kwamba moto huu utakuja kuwatambalia na wao pia."