Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, utawala haramu wa Israel hauna budi isipokuwa kusalimu amri mbele ya muqawama. Sheikh Nabil Qaouq amesisitiza kwamba, Harakati ya Muqawama wa Lebanon haina hofu yoyote ile ya kuingia vitani na utawala ghasibu wa Israel. Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameongeza kuwa, katika hali ngumu ya hivi sasa muqawama umeleta mlingano wa nguvu mpya na kwamba, Israel haina chaguo jingine ghairi ya kusalimu amri mbele ya muqawama wa wananchi. Sheikh Nabil Qaouq amesema bayana kwamba, endapo Israel itafanya kosa jingine la kijinga na kuanzisha vita vipya dhidi ya Lebanon, basi ijiandae kuvurumishiwa maelfu ya makombora ya muqawama ambayo yako tayari kwa ajili ya kufyatuliwa. Aidha amesisitiza kwamba, muqawama ni dharura ya kitaifa na stratejia kwa ajili ya kukabiliana na utawala adui wa Kizayuni.
HIZBULLAH: ISRAEL ISALIMU AMRI KWA MUQAWAMA.