CHANGAMOTO.


Tumebahatika kutembelea nyumba ya Bwana Muhammed Mputa, Mwanaharakati katika eneo la Chanika, ambaye nikiunganishi kikuu katika uwanja wa Tabligh, hususani kwenye Madhihabu ya Ahlul-Bayt (a.s), kwa kweli tumepata masikitiko sana kuona mahala anapoishi Mwanaharakati huyo ukilinganisha na kazi anayofanya, kwa kweli ni jambo la kusikitisha sana, kutokana na changamoto mbalimbali tunaitajika tuwe tunawaangalia watu wanaopigania dini ya Mwenyezi Mungu kwani wao ni watu muhimu sana katika jamii, Bwana Muhammed Mputa kwa kweli nyumba yake inamapungufu mengi sana, pia tumetembelea Madrasa yenye jina la Hassani Mujitaba kwa kweli ndugu msomaji unaweza kutokwa na machozi kutokana na eneo hilo kwa kutokuwa na viwango vya kuitwa Madrasa kwa kweli ni msiba mkubwa sijui leo hii Imam akidhihir tutasemaje kwa dhulma tunayowafanyia watu wa Chanika, atunabudi kushikamana kama Wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s) kuipigania Chanika, kufanya hivyo mafanikio yake yatakuwa makubwa mno katika eneo la Chanika na Madhihabu ya Ahlul Bayt (a.s) yatashika kwa kasi sana. Kwa yeyote ambaye yupo tayali kuchangia Madrasatul Hassan Mujtaba anaweza kuwasiliana na wausika kwa simu namba: 0786750004, 0712147889.

Mwenyezi Mungu anasema:
"Enyi mlioamini! mcheni Mwenyezi Mungu na mtu aangalie aliyoyatanguliza kwa ajili ya kesho, mcheni Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayoyatenda." (Qur'an: 59:18).

"Ndugu zangu huu ndio wakati wa vitendo zaidi sio maneno"